1. Kuwa Muadilifu

Uadilifu ni usimamizi wa ukweli na kutoa haki kwa kila anayestahiki kulingana na ukweli. Allah (s.w) ametuamrisha kuwa waadilifu kama ifuatavyo:Enyi mlioamini! Kuw eni wenye kusimamia uadilifu, mtoao ushahidi kwa ajili ya Allah ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu au wazazi au jamaa, akiwa tajiri au maskini, Mwenyezi Mungu anawastahiki zaidi. Basi msifuate matamanio mkaacha kufanya uadilifu. (4:135).Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi kwa ajili ya Allah, muwe mkitoa ushahida kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutowafanyia uadilifu. Fanyeni uadilifu, kufanya hivyo huwafanya kuwa wacha mungu. Na Mcheni Allah. Hakika Allah anajua mnayoyatenda (5:8)