Mnafiki ni yule anayeukubali Uislamu mdomoni (kwa kauli tu) lakini moyoni mwake na katika matendo yake anaukanusha. Wanafiki wanaainishwa vema katika aya zifuatayo:-
“Na katika watu wako wasemao: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Wanataka kumdanganya Allah na wale w alioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao, nao hawatambui.” (2:8-9)
Wanafiki pamoja na kuonyesha imani ya uwongo, ni maadui wakubwa wa Allah (s.w) na Mtume wake. Hushirikiana na Makafiri na Washirikina katika kuupiga vita Uislamu. Wao ni maadui wabaya zaidi kuliko makafiri na washirikina kwa sababu wao hutoa siri za ndani za Waislamu na kuwapelekea maadui wa Uislamu ili wapate kuuhilikisha Uislamu. Hivyo Allah (s.w) amewaahidi wanafiki kuwa watapata adhabu kali kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
Bila shaka wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto. Hutamkuta kwa ajili yao msaidizi’. (4:145)
Hakuna alama au nembo maalum zinazoonekana katika sura au viwili wili vya wanafiki, bali wanafiki wanatambulika kwa matendo
yao au mienendo yao. Mwenendo wa kinafiki au sifa za wanafiki zimebainishwa kwa uwazi katika Qur-an na Hadith Sahihi. Katika Qur’an Allah (s.w) amewaelelezea wanafiki katika aya zifuatazo:
(2:8-20), (3:167-168), (4:60-63), (4 :138-145), (9:43-68), (33:12-20), (57:13), (59:11-1 7), (63:1-8).
aya hizi tunajifunza kuwa wanafiki wamesifika kwa sifa
Maneno ya wanafiki siku zote ni kinyume na matendo yao.
Wanafiki hujaribu kumdanganya Allah pamoja na Waislamu wakidhani kuwa yaliyo vifuani mwao h ayaju likan i.
Hizi ndizo sifa za wanafiki kama zilivyobainishwa katika Qur-an. Kwa muhtasari, Mtume (s.a.w) anatufahamisha sifa za wanafiki kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatazo:
Mtume (s.a.w) amesema: Mambo manne akiwanayo mtu humfanya awe mnafiki wa wazi hata kama anaswali, anafunga na anadai kuwa ni Muumini,. Anayesema uw ongo kila anapoongea, anayevunja ahadi kila anapo ahidi, anayehini amana kila anapoaminiwa, na anayechupa mipaka kila unapotokea ugomvi. (Bukhari)
Muislamu wa kweli hana budi kujiepusha na unafiki kwa kujinasua na tabia za wanafiki.