Nini maana ya Uchoyo, na madhara yake kwenye jamii

31.

Nini maana ya Uchoyo, na madhara yake kwenye jamii

31. Kuepuka Uchoyo na Ubahili



Uchoyo na ubahili ni kinyume cha ukarimu. Mtu mchoyo ana kasoro katika imani yake. Anaona kuwa chochote alichonacho amekipata kwa jitihada na akili yake tu. Pia anahofu kuwa akitoa kumpa mwingine atapungukiwa au atafilisika. Mtume (s.a.w) anatutanabahisha katika Hadithi zifuatazo:



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Mtu anasema: “Hiki changu! Hiki changu! Lakini ukweli ulivyo ni kwamba, vilivyo vyake katika mali yake ni vitu vitatu: “Kile alichokula au nguo aliyoivaa ikachakaa au kile alichokitoa sadaqa (hakika) amekiweka akiba, na kingine chochote zaidi ya hivi, hakika si vyake (si vyenye kumfaa) na ataondoka awaachie watu ”. (Muslim)



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Chakula cha watu wawili kina watosha watu watatu, na chakula cha watu watatu kinawatosha watu wanne”.(Bukhari na Muslim)



Jabir bin Abdullah (r.a) ameeleza: Mtume w a Allah amesema: “Chakula cha mtu mmoja kinawatosha watu wawili na chakula cha watu wawili


kinawatosha watu wanne na chakula cha watu wanne kinawashibisha watu wanane”. (Muslim).
Hivyo ukizingatia Hadithi hizi, utaona kuwa hapana sababu ya Muislamu kuwa mchoyo au bahili. Uchoyo na ubahili ni tabia mbaya na malipo yake ni kwenda Motoni kama inavyobainishwa katika Qur-an:


Yule anayetoa (zaka na sadaka) na kumcha Mwenyezi Mungu. Na kusadiki jam bo jem a (akalifuata). Tutamsahilishia njia ya kw enda Peponi. Na afanyae ubakhili, asiwe na haja ya viumbe wenzake, na akakadhibisha mambo mema (asiyafanye). Tutamsahilishia njia ya kwendea Motoni. Na mali yake haitamfaa atakapokuwa anadidimia (Motoni humo). (92:5-11).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 2753

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

Husimamisha swala

Husimamisha swala katika maisha yao yote.

Soma Zaidi...
Zoezi

Maswali mbalimbali yanayohusu elimu ya dini ya kiislamu na mwongozo wa elimu na elimu mazingira.

Soma Zaidi...
(x)Wenye kuepuka lagh-wi

Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi.

Soma Zaidi...
Majina ya vijana wa pangoni

Makala hii inakwenda kukutajia majina ya vijana saba wa pangoni

Soma Zaidi...
Kwanini Ni muhimu kusimamisha uislamu katika jamii

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
sura ya 02

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...