24.
24. Kuwa na Haya
Kuwa na haya ni miongoni mwa tabia njema. Mtu mwenye haya ni yule anayejichunga na maovu na mambo ya aibu. Kuhusu umuhimu wa kuwa na haya, tunajifunza katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Haya ni sehemu ya imani na imani mahali pake ni Peponi; na uchafu (uovu) ni sehemu ya ugumu wa moyo na ugumu wa moyo mahali pake ni Motoni. (Ahmad, Tirmidh).
Ibn Mas ’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Miongoni mwa ujumbe watu waliopokea kutokana na mafundisho ya mwanzo ya Utume ni: Wakati unapokuwa huna haya, fanya ulitakalo. (Bukhari).
Hapa ina maana kuwa mtu asiye na haya hachagui la kufanya au la kusema. Pia Mtume (s.a.w) amesema katika Hadithi iliyosimuliwa na Imran bin Husain kuwa:
Haya haileti kitu kingine ila uzuri na katika maelelezo mengine; Haya ni nzuri katika kila hali. (Bukhari na Muslim).
Mtume (s.a.w) ambaye ndiye kiigizo chetu alikuwa ni mwenye haya sana kama Hadithi ifuatayo inavyobainisha:
Abu Said al-Khudri (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa na haya zaidi kuliko wasichana vigori ndani ya mitandio yao. Alipoona kitu kisichopendeza kwake tulikuwa tunakigundua kutokana na uso wake. (Bukhari na Muslim).
Muislamu anatakiwa awe na haya katika maongezi, katika kuangalia na katika kujisitiri uchi na katika kufanya kila jambo. Haya ni ngao ya kumuepusha mja na mambo maovu na machafu. Wa kwanza anayestahiki kuonewa haya ni Allah (s.w) kwani mwanaadamu hana kificho chochote cha kumsitiri asionekane kwake. Hivyo mja anayemuamini Allah (s.w) atamuonea haya na kujiepusha na maovu na machafu katika maisha yake yote popote atakapokuwa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 583
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Kitabu cha Afya
(xvi)Huepuka ugomvi na mabishano
Waumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano. Soma Zaidi...
Kitabu Cha Quran na sayansi
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...
Assalam Baada yakufariki wazazi wake mtume alilelewa nanani???
Mtume Muhammad s.a.w amezaliwa yatima asiyena baba. Lakini hii haikumfanya asipate maelezo bora yaliyo mazuri. Je unajuwa aliyemlea baada ya kufariki kwa mama yake?. Soma Zaidi...
(xiii)Huwa muaminifu
Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Elimu
Uwanja wa elimu na maarifa Soma Zaidi...
jamii somo la 26
(vii)Hufanya bias hara na Allah (s. Soma Zaidi...
UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...
Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake
30. Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Funga
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...