ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli
Ukweli ni uhakika wa jambo.
-
Kuwa Mkweli
Ukweli ni uhakika wa jambo. Muislamu wa kweli hana budi kuwa mkweli na kusimamia ukweli. Allah (s.w) anatuamrisha tuwe wakweli katika kuendesha shughuli zetu zote.
“Enyi mlioamini Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (9:119).
Msema kweli ni mpenzi wa Allah (s.w) . Naye Allah (s.w) amewaandalia wakweli ujira mzuri kabisa kwa hapa duniani na huko akhera kama tunavyobainishiwa katika Qur-an” kuwa Allah (s.w) atasema katika hiyo siku ya hisabu:-
“Hii ndiyo siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata bustani zipitazo mbele yake mito. Humo watakaa milele. Allah amewawia radhi nao wanaradhi naye. Huku ndiko kufaulu kukubwa. (5:119)
“... Na wanaume wasemao kweli na wanawake wasemao kweli... Allah amewaandalia msamaha na ujira mkubwa”. (33:35).
Msisitizo wa Muislamu kujipamba na tabia ya kuwa mkweli pia tunaupata katika Hadith ifuatayo:
‘Abdullah bin Mas ’ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Utaongea ukweli kwa sababu ukweli unaongoza kwenye Ucha-Mungu na Ucha-Mungu unaongoza kw enye Pepo. Mja ataendelea kusema kweli na kubakia katika ukweli mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa wakweli wakubwa.Tahadharini na uwongo! Uwongo unaongoza kwenye uasi na uasi unaongoza kwenye Moto.Mja ataendelea kusema uwongo na kubakia katika uwongo mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa waongo wakubwa”.
(Bukhari na Muslim).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Dua za Mitume na Manabii π2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π3 kitabu cha Simulizi π4 Bongolite - Game zone - Play free game π5 ai web app π6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Athari na faida za kumuamini Allah katika maisha ya mwanadamu duniani na akhera
Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.
Soma Zaidi...