Kujiepusha na Ria na Kujiona

Ria ni kinyume cha Ikhlas. Kufanya ria ni kufanya jambo jema ili watu wakuone, wakusifu, wakupe shukurani, n.k. Mtu anayefanya ria hafanyi wema kwa kutarajia malipo kutoka kwa Allah (s.w) bali hufanya kwa kutarajia malipo ya hapa duniani tu, iwe ni mali au sifa au shukurani.

Mwenye kufanya ria hata akijiita Muislamu hana malipo yoyote mbele ya Alllah(s.w) katika siku ya Hukumu isipokuwa adhabu kali Motoni kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:-“Wanaotaka maisha ya dunia na mapambo yake, tutawapa huku duniani (ujira wa) vitendo vyao kamili, humu wao hawatapunjwa. Hao ndio ambao hawatakuwa na kitu katika akhera ila moto na wataruka patupu waliyoyafanya katika dunia hii na yatakuwa bure waliyokuwa wakiyatenda.” (11:15-16)

Katika aya nyingine Allah (s.w) anatukamia:“Basi adhabu (kali) itawathubutikia wanaoswali; ambao wanapuuza swala zao. Ambao hufanya riyaa ”. (107:4)

Katika Hadith tunafahamishwa kuwa Mtume (s.a.w) amesema:

“Katika siku ya hukumu, vitendo vyote vilivyofanywa hapa duniani vitahudhurishwa mbele ya Allah (s.w). Vitendo vilivyofanywa kwa ajili ya Allah (s.w) vitatengw a. Na vitendo vingine vilivyofanyw a kw a nia nyingine mbali mbali vitatupw a motoni”. (Baihaqi).