picha

kuwa na ikhlas

Ikhlas ni kufanya kila jambo jema kwa ajili ya Allah (s.

kuwa na ikhlas
  1. KUWA NA IKHLAS

Ikhlas ni kufanya kila jambo jema kwa ajili ya Allah (s.w) tu. Yaani kutoa huduma na mali kwa watu wanaohitajia msaada bila ya kutaraji malipo yoyote kutoka kwao ila kutoka kwa Allah (s.w) tu. Kwa mfano kumlisha na kumvisha fukara, maskini au yatima bila ya kutarajia hata kupata shukurani (ahsante) kutoka kwake ila tu kwa kutegemea malipo kutoka kwa Allah (s.w) ni kitendo cha Ikhlas. Wale wanaotoa misaada



kwa wanaohitajia kwa Ikhlas, wamesifiwa na Allah (s.w) katika Qur-an:



“Na huwalisha chakula maskini na yatima na wafungwa na hali yakuwa wenyewe wanakipenda (chakula hicho. Husema nyoyoni mwao wanapowapa chakula hicho): Tunakulisheni kwa ajili ya kutaka radhi ya Mw enyezi Mungu (tu). Hatutaki kw enu m alipo w ala shukurani. Hakika sisi tunamuogopa Mola wetu hiyo siku yenye shida na taabu.”

(76:8-1 0).



“Na amchaye (Mwenyezi Mungu) ataepushwa nao (huo moto uwakao kwa nguvu). Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa na hali ya kuwa hakuna yeyote anayemfanyia ihsani ili awe anamlipa. Isipokuwa (anafanya haya) kwa kutaka radhi ya Mola wake Mtukufu. Basi atapata la kumridhisha.” (92:1 7-21).

Si katika kutoa tu mali, bali lolote lile analolifanya Muislamu wa kweli hana budi kulifanya kwa nia ya kupata radhi ya Allah (s.w). Utendaji wa Mwanaadamu uliofanywa kwa Ikhlas ndio tu utakaomuwezesha kuwajibika vilivyo kwa wanaadamu wenzake na kwa Mola wake Mtukufu.

Ili kujikumbusha mara kwa mara kufanya mambo yetu kwa Ikhlas, ni Sunnah kila tunapoanza swala kabla ya kusoma Suratul-Fatiha tu seme:

“Ninauelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, hali ya kuwa nimewacha dini za upotofu mimi (nimejisalimisha ni Muislamu na ) si miongoni mwa washirikina. (6:79)



Hakika swala yangu, na ibada zangu (zote nyingine) na uzima wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Bwana wa walimwengu wote. Hana mshirika wake na kwa haya ndiyo niliyoamrishwa,na mimi ni wa kwanza wa waliojisalimisha. (6:162-163)



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views 2960

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 web hosting     👉5 ai web app     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Al-Arba'uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 1: Nia

huu ni mwanzo wa kitabu hiki cha Matn arbaina Naway

Soma Zaidi...
DUA YA MUUMINI NA DUA YA KAFIRI

DUA YA KAFIRI NA DUA YA MUUMINI.

Soma Zaidi...
UHAKIKI WA HADITHI

Uhakiki wa Hadith za Mtume (s.

Soma Zaidi...
DUA ZENYE MANENO HAYA HUJIBIWA

SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.

Soma Zaidi...
Fadhila za udhu yaani faida za udhu

Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu

Soma Zaidi...