huu ni mwanzo wa kitabu hiki cha Matn arbaina Naway
Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika (kusihi kwa) ‘amali kunategemea niyyah, na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokinuia. Kwa hiyo ambaye hijrah yake ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, basi hijrah yake ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake. Na ambaye hijrah yake ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (fulani), basi hijrah yake ni kwa lile aliloliendea.”
[Hadiyth hii imepokelewa na Maimaam wawili ‘Ulamaa wa Hadiyth, Abuu ‘Abdillaah Muhammad bin Ismaa’iyl bin Ibraahiym bin Al-Mughiyrah bin Bar-dizbah Al-Ju’fiyy Al-Bukhaariy, na Abul-Husayn Muslim bin Al-Hajjaaj bin Muslim Al-Qushayriyy An-Naysaaburiyy (Rahimahuma-Allaah) Wameipokea katika vitabu vyao ambavyo ndio Swahiyh katika vitabu vya Hadiyth vilivyosanifiwa]
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu haki za Muislamu kwa Muislamu mwenzie
Soma Zaidi...Wapo watu kadhaa ambao waliomba dua hazirudi. Hapa nitakueleza wawili ambao ni mzazi na msafiri.
Soma Zaidi...