kuwa mwenye hikma au hekima na faida zake

Elimu, pamoja na ubora wake, hainufaishi bila ya kutumiwa kwa hekima.

kuwa mwenye hikma au hekima na faida zake

2. Kuwa na Hekima

Elimu, pamoja na ubora wake, hainufaishi bila ya kutumiwa kwa hekima. Kufanya jambo kwa hekima ni kufanya jambo kwa kutumia ujuzi unaostahiki na kwa kufuata utaratibu unaostahiki kulingana na mahali na wakati kwa kuzingatia mwongozo na mipaka ya Allah (s.w) na Sunnah ya Mtume wake.



Kila Muumini anawajibika kufanya mambo yake yote kwa ujuzi wa kutosha. Kabla Muislamu hajafanya jambo lolote anatakiwa afahamu len

go la hilo analolifanya na je, hilo lengo linampelekea kumuabudu Mola wake na kuwa Khalifa wake au la. Baada ya kulifahamu lengo hanabudi kuwa na ujuzi na mbinu zinazostahiki kumfikisha kwenye lengo kwa wepesi na kwa ufanisi. Asichague njia ndefu na ngumu akaacha njia fupi na nyepesi inayowafikiana na mwongozo wa Allah (s.w) na Sunnah za Mitume wake.



Hekima ni katika vipengele vya tabia njema vilivyo azizi anavyotakiwa avipiganie Muumini ili awe na hadhi inayostahiki, hadhi ya Ukhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni. Waumini hatuna budi kufanya mambo yetu kwa hekima na daima tumuombe Allah atuzidishie Hekima.



“(Allah) Humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa heri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili.” (2:269).



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 943

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

MASHARTI YA KUKUBALIWA KWA DUA

MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.

Soma Zaidi...
Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.

Soma Zaidi...
DUA na Adhkar kutoka kwenye quran

hii ni orodha ya dua mbalimbali kutoka kwenye quran. Unaweza kuzitumia dua hizi kujipendekeza kwa Allah na kupata msamaha, neema na mengineyo.

Soma Zaidi...
hadithi ya 8

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى ?...

Soma Zaidi...
Je! inajuzu wanawake kuzuru makaburi?

As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, nauliza inajuzu wanawake kuzuru makaburi?

Soma Zaidi...