UHAKIKI WA HADITHI

Uhakiki wa Hadith za Mtume (s.

UHAKIKI WA HADITHI

Uhakiki wa Hadith za Mtume (s.a.w)
Kwa kuwa Hadith hazikuwa na ahadi ya Allah (s.w) ya hifadh kama ilivyo kwa Qur-an - "Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha haya (Qur-an) na hakika sisi ndio tutakaoyalinda". (15:9) - walitokea watu waovu wakamzulia Mtume (s.a.w) mambo mengi yaliyokinyume kabisa na Uislamu wenyewe.Β  Hili liliwastua wanazuoni wacha-Mungu na kuwafanya wawajibike kuweka utaratibu maalumu wa kuchambua Hadith za Mtume (s.a.w). Katika harakati za uchambuzi wa Hadith, wanazuoni wa Hadith waliigawa Hadith katika sehemu kuu mbili - Isnad na Matin.

Isnad ni sehemu ya Hadith inayoonyesha msururu wa wapokezi wa Hadith hiyo tokea kwa yule aliyemsikia Mtume (s.a.w) akieleza jambo au aliyemuoma Mtume akifanya jambo, au aliyemuona Mtume akiridhia au akithibitisha jambo lililofanyika mbele yake au akieleza tabia ya Mtume (s.a.w) kama alivyoiona.
Mfano wa Isnad:
AmetuHadithia Abdallah bin Yusuf toka kwa Malik toka kwa Abizinadi toka kwa A'araji toka kwa Abu Hurairah ambaye amesema: Hakika ya Mtume wa Allah (s.a.w) amesema: ……………." (Bukhari) Kwa hiyo msururu wa watu wote hao kuanzia yule aliyemsikia Mtume (s.a.w), Abu Hurairah (r.a) ambaye ni sahaba wa Mtume, hadi kumfikia Bukhari ambaye ni Imamu wa Hadith aliyeipokea na kuiandika ndio Isnad.Β 

Matin ni kauli ya Mtume au matendo yake.
Mfano wa Matin:
Mtume (s.a.w) amesema: β€œYule ashikaye silaha dhidi yetu si pamoja na sisi." (Muslimu) Maneno aliyosema Mtume (s.a.w) yaliyofungiwa kwenye "…………………….." ndio matin ya Hadith hii. Riwaya Matin moja ya Hadith inaweza kuripotiwa na msururu wa wapokezi (Isnaad) zaidi ya moja.
Kwa mfano:
Mtume (s.a.w) amesema "Yule ashikaye silaha dhidi yetu si pamoja sisi." (Muslimu) Maneno haya aliyosema Mtume (s.a.w) yamesimuliwa katika riwaya tatu zifuatazo:
1. β€œAbdullah bin Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yule ashikaye silaha dhidi yetu si pamoja na sisi." (Muslimu)

2. Ilyas bin Salama ameHadith a kutoka kwa baba yake kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yule ashikaye upanga (silaha) dhidi yetu si pamoja na sisi." (Muslimu)

3. Abu Musa Ashiari amesema kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yule ashikaye silaha dhidi yetu si pamoja na sisi. (Muslimu)

Uhakiki wa Isnad
Katika harakati za kuchuja Hadith zilizosahihi na zisizo sahihi; wanazuoni wa Hadith walikuwa wakifuatilia kwa undani historia ya wale wote waliomo kwenye msururu wa wapokezi wa Hadith na kumchunguza mtu wa kwanza kuHadith a Hadith hiyo kuwa kweli alikuwa Swahaba balegh na Mkalafi aliyekuwa na uwezo wa kumsikia au kumuona Mtume (s.a.w).Β 

Kwa ujumla, ili Hadith iwe sahihi, kila msimulizi katika Isnad alitakiwa awe Muislamu mwaminifu, mwenye kumbukumbu nzuri, mwenye tabia njema na mcha-Mungu.

Uhakiki wa Matin
Pamoja na kuwa na usahihi katika upokezi wa Hadith, "Matin" ya Hadith inaweza isiwe sahihi. Hivyo Hadith itakuwa shihi iwapo sehemu zote kwa pamoja - Isnad na Matin vitakuwa sahihi. Matin ya Hadith itakuwa sahihi iwapo itatekeleza masharti yafuatayo:
(i) Isipingane na Qur-an.
(ii) Isipingane na Hadith nyingine iliyothibitishwa kuwa ni sahihi.
(iii) Isimzulie Mtume (s.a.w) kufanya jambo ambalo ni kinyume na Uislamu.
(iv) Isipingane na hakika (fact)
(v) Isipingane na ukweli unaothibitishwa na historia.
(vi) Isiwe na maneno ya uongo ndani yake.
(vii) Isiwe inaahidi adhabu kali sana kwa kosa dogo sana na isiwe imeahidi malipo makubwa sana kwa wema mdogo sana.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 1181

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Al-Arba-uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 5: kujiepusha na uzushi katika dini

Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini

Soma Zaidi...
DUA ZENYE MANENO HAYA HUJIBIWA

SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.

Soma Zaidi...
MASHARTI YA KUKUBALIWA KWA DUA

MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.

Soma Zaidi...
AINA ZA HADITHI

Aina za HadithKuna aina kuu mbili za Hadith- (a) Hadith Nabawiyyi.

Soma Zaidi...
Maana ya dua na fadhila zake

Dua ni moja ya Ibada ambazo tunatakiwa kuziganya kila siku. Kuna fadhila nyingi sana za kuomba dua. Post hiibitakwenda kukujuza fadhila za kuomba dua.

Soma Zaidi...