ZIJUWE NAMNA ZA KUZUIA HASIRA, NA MADHARA YA HASIRA
28.
28. Kudhibiti Hasira
Kujizuia na hasira ni tabia njema inayoambatana na tabia ya kusamehe. Hasira humpata mtu anapoudhiwa. Wakati mwingine huja ghafla na kumnyima mtu wakati wa kufikiri. Hasira zinaongozwa na shetani, hivyo humnyima mtu nafasi ya kutumia akili, hekima na busara. Hivyo humpelekea mtu kufanya matendo ambayo hugeuka kuwa majuto baadaye. Hasira hasara. Kujizuilia na hasira ni kitendo cha ucha Mungu chenye malipo makubwa mbele ya Allah (s.w). Rejea Qur-an (3:133-134) na (42:36-37). Pia ubora wa kujizuilia na hasira unadhihirika katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah(r.a) am esim ulia kuw a m tu mm oja alim uom ba Mtum e (s.a.w): “Niwaidhi’. Mtume akasema: “Usighadhibike”. Kisha akarudia mara nyingi akisema: Usighadhibike. (Bukhari)
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema “Mtu mwenye nguvu si bingwa wa mieleka bali mtu mwenye nguvu ni yule anayejizuilia na has ira ”. (Bukhari na Muslim).
Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Hapana mja aliyemeza kidonge kichungu mbele ya Allah (s.w) kuliko kidonge cha hasira alichokimeza, huku akitaraji radhi ya Allah (s.w)”. (Ahmad).
Mbinu za kujizuia na hasira zimebainishwa katika Qur-an kama ifu atavyo:
“Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze majahili (wajinga). Na kama wasi wasi wa shetani ukikusumbua basi (sema: Audhubillah) jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Bila shaka yeye ndiye asikiaye na ajuaye.” (7:199-200).
Kutokana na aya hizi
hasira ni hizi zifuatazo:
(i) Kushikamana
(ii) Kushikamana
(iii) Kuwapuuza m
(iv) Kujikinga kwa tunajifunza kuwa mbinu za kujizuilia na
na kusamehe.
na kuamrisha mema.
ajah ili.
Allah (s.w) na uovu wa shetani.
Pia Mtume (s.a.w) anatupa mbinu nyingine za kupambana na hasira katika Hadithi zifuatazo:
Atiyyah bin Urw ah Ba ’id(r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah amesema: “Hakika hasira zinatoka kwa Shetani, na Shetani ameumbwa kutokana na moto na hakika moto huzimishwa na maji. Kwa hiyo yoyote miongoni mwenu atakayepandwa na hasira, na atawadhe”. (Abu Daud).
Abu Dharr (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Wakati wowote mmoja wenu atakapopandwa na hasira akiwa amesimama, na akae chini. Kama (kwa kufanya hivyo) hasira itamtoka ni vyema; lakini kama haitatoka, na alale chini”. (Ahmad, Tirmidh).
Kutokana na Hadithi hizi Mtume (s.a.w) anatuelekeza tupunguze hasira zetu kwa:
(i)Kutia udhu.
(ii)Kukaa chini iwapo tumesimama.
(iii)Kulala chini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 web hosting 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 ai web app 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 3: Nguzo za uislamu
Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu
Soma Zaidi...Jinsi ya Kuswali Swala ya Tahajjud
Katika makala hii utajifunza maana ya Swala ya Tahajjud, umuhimu wake, wakati unaofaa wa kuiswali, jinsi ya kuiswali hatua kwa hatua, idadi ya rakaa, dua zinazofaa kuomba baada ya swala, pamoja na makosa ambayo baadhi ya watu huyafanya wanapotekeleza ibada hii.
Soma Zaidi...Muangalie aliye chini yako na usimuangalie aliye juu
Katika hadithi hii utakwenda kujifunza hekma ya kuangalia watu walio chini yako na sio walio juu yako
Soma Zaidi...