DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.
![]()
![]()
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI
Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Hakuna haja ya kumeza dawa za kupunguza maumivu kwa mwenye kumuamini Allah. Ila watu wasielewe vibaya maneno haya, maaana Mtume (s.a.w) amesisitiza watu wajitibu, ila pia ieleweke Allah amejaalia kuwa qurani ni dawa na ni ponyo kwa maradhi na mabo mengine. Leo hapa nimewaandalia dawa ya kuondowa maumivu katika sunnah nayo ni dua ambayo mtume (s.a.w) alikuwa akiwafundisha masahaba waombe pindi wakiwa na maumivu na maradhi.
1.Mtume (s.a.w) alimwambia swahaba kuwa: âweka mkono wako pale unaposikia maumivu katika mwili wako kisha sema âBISMILLAHIâ mara tatu kisha useme mara saba (maneno haya): âAâUDHU BILLAHI WAQUDRATIHI MIN-SHARI MAA AJIDU WA-UHAADHIRUâ. Hadithi hii ni sahihi na amepokea Muslim, Abu Daud na Ibn Maajah kutokana na masimulizi ya âUthman Ibn Abil-âAs.
2.Mtume (s.a.w) alimwambia Mainuna bint Abi Ubay kuwa :âweka mkono wako wa kulia pale panapokupatia maudhi (maumivu) kisha sema âBISMILLAHI ALLAHUMMA DAAWINI BIDAWAAIKA WASHFINII BISHAAIKA WAGHANII BIFADHLIKA âAN-MAN SIWAAKA WAHDHUR âANII ADHAAKAâ (Amepokea Tabrany)
3.Mume (s.a.w) alimwambia Asmaa bint AbuBakar kuwa: âweka mkono wako (pende maumivu) na useme mara tatu âBISMILLAHI ALLAHUMMA ADH-HAB âANNI SHARRA MAA AJIDU BIDAâAWATIKA NABIYYIKA TWAYYIBIL-MUBAARAKIL-MAKIIN âINDAKA. BISMILLAHI â (Amepokea ibn âAsakir)
4.amesimulia Ibn âAbas (r.a) kuwa : âalikuwa Mtume (s.a.w) akitufundisha dua kwa ajili ya maradhi na maumivu yote tunayoyapata kuwa Mtu aseme: âBISMILLAHI, AâUDHUBILLAHIL-âADHIIM MINSHARRI KULLI âARQIN-NAâAARI, WAMINSHARRI HARRIN-NAHAARIâ (Amepokea Ahmad, tirmidh na Alhaakim).
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakufundisha dua za kuomba wakati wa woga, wasiwasi na kujikinga na wachawi na mashetani
Soma Zaidi...DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya hadithi al Quds na Hadith an-Nabawiy
Soma Zaidi...