DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 1.
DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI
1.Kutaka hifadha dhidi ya vitimbi vya shetani na wasiwasi ni jambo ambalo Allah ametuamrisha kulifanya. Hivi pia ndivyo ambavyo mtume wetu alikuwa akifanya. Amesema Allah (s.w): “Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.” Quran surat al-an-muumin aya ya 97-98).
Hivyo hapa tunajifunza kuwa ukitaka kujikinga na wasiwasi na vitimbi vya shetani unatakiwa useme maneno haya aliyotufundisha Allah (s.w) ambayo ni kusema “RABBI A’UUDHUBIKA MIN-HAMAZAATISH-SHAYAATWIN, WA A-’UUDHUBIKA AN-YAHDUDUUN” katika dua hii herufi D hap utaona imepigiwa msitari. Hiyo ni herufi ض ambayo hainna mwenzie kwenye kiswahili. Fatilia kwa wasomi wakufundishe inavyosomwa. Kwa kiarabu dua hii ni hii chukua msahafu wako fungua surat al-muumin aya ya 97-98
وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ ﴿٩٧﴾ وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ ﴿٩٨﴾
2.mwenye kutaka kuikinga nyumba yake na mwili wake pamoja na ahali zake dhidi ya uchawi na majini masi asome surat al-baqara japo mara moja kila baada ya siku tatu, au asome ayat al-qursiy na aya mbili za mwisho za surat al-baqara japo mara moja kwa siku au asubhi na jioni. Au asome sura al-mu’awidhatayn yaani surat al-falaq na surat an-na sura hizi asome pamoja na surat al-ikhlas kwa utaratibu aloufanya Mtume (s.a.w), tutauzungumza hapa. Hebu tuone kwanza faida za sura hizi kwa mapokezi ya hadithi zilizo sahihi
1.Surat al-fatiha.
Amesimulia Ibn ‘Abas kuwa “wakati ambao jibril alikuwa amekaa na Mtume akasikia sauti ya mlango uliofunguliwa juu yake akanyanyu kichwa chake kisha akasema “hiyo ni nsauti ya mlango uliopo mbinguni umefunguliwa siku ya leo, na katu haujawahi kufunguliwa ila ni leo tu (ndio mara ya kwanza kufunguliwa).
Basi akashuka Malaika kutoka kwenye mlango huu akasema (Jibril) huyu ni malaika ameshuka duniani na hajawahi kushuka kamwe ila ni leo tu akatoa salamu (malaika huyo) kisha akasema (kumwambia mtume) tuo habari za furaha kwa nuru mbili ulizopewa na hakuwahi kupewa mtume yeyote kabla yako kamwe (ambazo ni) surat al-fatiha na aya za mwisho za surat al-baqarah hatusoma herufi yeyote isipokuwa utapewa” (amepokea Muslim).
Amesema Mtume “surat al-fatiha ni dawa ya kila gonjwa” amepokea Bayhaqiy)
2.surat al-baqarah
Amesema Mtume “…Mwenye kuisoma katika nyumba yake usiku hatoingia shetani nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu, na mwenye kuisoma mchana hatoingia shetani nyumba hiyo kwa michana mitatu” (amepokea Ibn hiban, tabrany na Bayhaqiy). 3.ayat al-qursiy.
Amesema Mtume “katika surat al-baqarah kuna aya iliyobora kuliko aya zote haitasomwa aya hiyo kwenye nyumba yenye shetani ila atatoka kwenye nyumba hiyo, (aya hiyo ni) ayat al-kursy) (amepokea Al-Haakim na Bayhaqiy)
3.aya za mwisho za surat al-baqarah
Amesema Mtume hakika Allah ameimalizia surat al-baqarah kwa aya zilizo tukufu (zilizotoka) kwenye hazina chini ya ‘arshi basi jifundisheni aya hizo na muwafundishe wake zenu na watoto wenu. Kwani mna ndani ya aya hizo dua, qiraa na dua” (amepokea Al-Haakim kutoka kwa Abuu Dhari).
Pia Amesema mtume “aya mbili za mwisho za surat al-baqarah mwenye kuzisoma usiku zitamtosheleza” (amepokea bukhari,Muslim,Ahmad na Ibn Maajah kutoka kwa ibnmas’ud)
4.Suratul ikhlas, nasi na falaq
Amesimulia ‘Abdallah Ibnhabib kuwa Mtume amesema “QUL HUWA LLAHU AHADU na mu’awadhatayn (qul a’udhu birabin-nasi na qul a’udhu birabil-falaq) (mwenye kuzisoma ) asubuhi na jioni zinatosheleza kwa kila kitu.(amepokea ahmad, Tirmidh na Nisai).
Hizi ni baadhi tu ya sura mahususi ambazo Mtume alikuwa akiwasisitiza masahaba zake wazisome. Sura nyingine ni kama al-imran, al-an’am, al-israa, al-kahaf, surat musabahat(sura zilizoanzwa na tasbih nnazo zipo saba), surat al-mulkk, surat ar-rahman, surat al-waqi’a, surat al-zalzala, surat at-takathur, surat al-fiyl, surat al-kafiruun, surat yasin n.k. Kupata faida zaidi ya sura hizi download App yetu iiitwayo darsa za quran, utafaidiza zaidi.
Sasa hebu tuone namna ambavyo Mtume (s.a.w) katika maisha yake tunapata mafunzo alivyokuwa akitumia sura hizi kama ni kinga na dawa kwa mambo mbalimbali:-
1.Mtume (s.a.w) amesema:”mwenye kusoma aya kumi nne za mwanzo katika surat al-baqarah, na ayat al-qursiy na aya mbili baada ya aya hii, na aya mbili zilizo mwishoni mwa surat al-baqarah hataingia katika nyumba hiyo shetani mpaka asubuhi” (amepokea hadithi tabrany na Alhakim akaisahihisha).
2.Mtume alikuwa anapokwenda kulala anasoma sura na aya hizi, kwa utaratibu huu:-
Alikuwa Mtume (s.a.w) akienda kulala usiku, akiweka pamoja viganja vyake kisha akivipulizia na akivisomea suratul-Ikhlas, suratul Falaq na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani, usoni na mbele (akifanya hivyo mara tatu.) (Bukhari na Muslimu)
Mtume (s.a.w) amesema: "Ukienda kulala soma Ayatulkursiyyu kwani Allah ataendelea kukuhifadhi, wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi." (Al-Bukhari)
Mwenyezi Mungu, hakuna Mola ila yeye, ndiye mwenye uhai wa milele, msimamia kila jambo. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni vyake (peke yake vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na (yaliyo) nyuma yao; wala (hao viumbe) hawalijui lolote katika ilimu yake ila kwa alipendalo. Enzi yake imeenea mbinguni na ardhini, wala kuvilinda hivyo hakumshindi; Na yeye (pekee) ndiye aliye juu na ndiye aliye mkuu." (2:255)
Alikuwa Mtume (s.a.w) akitaka kulala, anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake, kisha anasema: "Allahumma qiniy a'dhaabaka yaumatab-a'thu i'baadaka." "Ee! Allah nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakapowafufua waja wako."
Pia Mtume (s.a.w) wakati wa kulala alikuwa akisema: “Allahumma Bismika amuutu wa-ahyaa. “Kwa jina lako, Ee Allah ninakufa na nina kuwa hai." uzi na ndiye Mwenye hikima (2:32)
3.Dua pindi uonaposhetani au unapotishwa na shetani
Ikitokea Mtu ameona shetani au ametishwa na shetani anatakiwa kuleta isti’adha na asema “A’UDHU BILLAHI MINKA” mara tatu kisha aseme “AL-’ANUKA BILA’ANATIL-LLAHI TAAMMAH” mara tatu. Hakika shetani anakimbia ukisema maneno hayo. Hatika mapokezi ukimuona shetani akikutisha au hakukutisha soma adhana hakika shetani hukimbia adhana. Katika hadithi alopokea muslim mtume (s.a.w) amesema “hakika shetani hukimbia pindi adhana ya swala inaposomwa”
Kwa ufupi zipo dua nyingi lakini qurani inatosha kabisa kufanya kila tunalolitaka. Qurani inatosha kuwa kinga ya wachawi, majini na vijicho. Dua zaidi tumeziwekakwenye App yetu iitwayo swala na dua. Tumeweka kule kwa kuhofia kuirefusha app ii kuwa ndefu zaidi. Tunasikiliza mawazo yenu wasomaji zaidi. Kuiboresha App hii. Darsa hii imewekwa kutegemea na michango na maoni ya masomaji wetu. Tutaendelea kufanya hivu zaidi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 528
Sponsored links
👉1
Kitabu cha Afya
👉2
Madrasa kiganjani
👉3
Simulizi za Hadithi Audio
👉4
Kitau cha Fiqh
👉5
kitabu cha Simulizi
👉6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Masharti ya kukubaliwa kwa dua
Post hii itakwenda kukugundisha masharti yanayofungamana na kukubaliwa kwa dua. Soma Zaidi...
Al-Arba uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 7: Nasaha katika dini
Post hii itakufundisha umuhimu wa nasaha katika dini Soma Zaidi...
UHAKIKI WA HADITHI
Uhakiki wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...
KATU USITAMANI MAUTI (KIFO) YAANI KUFA, HATA UKIWA NA MARADHI AMA UKIWA MCHAMUNGU UKIWA NI MUOVU MTENDA MADHAMBI MAKUBWA NA MADOGO
Soma Zaidi...
Matamshi ambayo ukimwambia Allah kwenye dua yako basi hujibiwa kwa haraka dua hiyo
Post hii inakwenda kukufundisha matamshi ambayo mtu akiyatamka Allah hujibu dua hiyo kwa urahisi. Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...
hadithi ya 8
عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى ?... Soma Zaidi...
dua ya kuomba jambo ufanikiwe
hii ni damna ya kuomba dua ukubaliwe, dua ya kuomba jambo ufanikiwe Soma Zaidi...
Vyanzo vitano vya elimu zote duniani: Chanzo cha Elimu ni Allah (s.w)
Kama tunavyojifunza katika surat ‘Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s. Soma Zaidi...
DUA ZA SWALA
DUA ZA SWALA 1. Soma Zaidi...