Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudi kumfanya Mtume (s.a.w) kuwa kiigizo chake kimwenendo na kitabia. Mtume (s.a.w) alikuwa na tabia njema kabisa kama tunavyofahamishwa katika Qur’an:
“Na bila shaka (Wewe Muhammad) una tabia njema kabisa.” (68:4) |
Mtume (s.a.w) mwenyewe amewahimiza waumini kujipamba na tabia njema kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Abdullah bin Amr (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Aliye kipenzi changu kuliko wote katika nyinyi (Wa is lam u) ni yule aliyew azidi kwa tabia njema”. (Bukhari)
Harithat bin Wahab (r.a) ameeleza kuwa Mtume w a Allah amesema: “Yule ambaye tabia yake ni mbaya na katili, hataingia Peponi”. (Abu Daud)
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah amesema: “Mw enye imani iliyopea katika Waislamu ni yule mwenye tabia njema, na aliye mbora katika nyinyi ni yule anayemtendea wema mkewe”. (Tirmidh)
Abu Darda (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Hapana kitu kitakachotia uzito katika m izani ya Muum ini katika siku ya hukum u kuliko tabia njema...” (Tirmidh)
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliulizwa juu ya mambo yatakayopelekea watu wengi kuingia Peponi. Alijibu Mtume: “Uchaji - Mungu na tabia njema”. Kisha akaulizwa tena: “Ni mambo yepi yatakayompelekea m tu kuingizw a Motoni? ” Alijibu Mtum e, “Mdom o n a tup u (viungo vy a s iri)”. (Tirm idh)
Hivyo, muumini wa kweli hanabudi kujipamba na vipengele vya tabia njema vilivyoainishwa katika Qur-an na Sunnah. Katika juzuu hii
tumerejea vipengele vya tabia njema vifuatavyo: