Usawa na uhuru wa kuchuma mali katika uislamu
Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali.
Haki na Uhuru wa kuchuma katika Uislamu
Kwa kuwa kuchuma kwa njia za halali ni wajibu kwa kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, hapana budi kila mtu kupewa uhuru kamili wa kutumia juhudi yake na vipawa vyake katika kuchuma kwa njia za halali. Katika Uislamu ni kosa kubwa kwa serikali au Dola kuweka vikwazo vya kuwazuia watu wasitumie vipaji vyao na uwezo wao wote katika kuchuma kwa njia za halali. Kinyume chake, serikali au dola ya Kiislamu ina wajibu wa kuondoa vikwazo vyote vinavyowazuia watu kutumia vipawa vyao vyote katika kuchuma na inawajibu pia wa kutoa motisha na vishawishi vya kuwavutia watu binafsi au watu waliojiunga katika vikundi wajiingize katika sekta mbali mbali za uchumi kwa juhudi kubwa na maarifa.
Pamoja na uhuru kamili uliotolewa na Uislamu wa kuchuma kwa njia za halali kwa kadri ya uwezo wa kila mtu, pia unampa kila mtu haki ya kumiliki kila alichokichuma kwa njia za halali kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
“Wala msitamani vile ambavyo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma, na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma. Na mwombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mjuzi w a kila kitu. (4:32)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina ๐2 Kitau cha Fiqh ๐3 Simulizi za Hadithi Audio ๐4 Dua za Mitume na Manabii ๐5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) ๐6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Aina au migawanyo mbalimbali ya haki katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sifa za kuwa maamuma kwenye swala na namna ya kumfuata imamu
Post hii inakwenda kukuelezea sifa za kuwa maamuma na taratibu za kumfuata imamu.
Soma Zaidi...Hatua za kinga za ugumba na Utasa.
Ugumba ni รขโฌลugonjwa wa mfumo wa uzazi unaofafanuliwa kwa kushindwa kupata ujauzito baada ya miezi 12 au zaidi ya kujamiiana bila kinga mara kwa mara. Utasaรย kutoweza kwa kiumbe hai kufanya uzazi wa ngono au kutoweza kupata mimba au kuchangia mimba.
Soma Zaidi...