Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu

Kutoa Shahada Mbili

Kwa mujibu wa Hadith, tuliyoirejea katika utangulizi, nguzo ya kwanza ya Uislamu ni kutoa shahada mbili kwa kusema:



Ash hadu an laailaha illa llaahu wa ash hadu anna Muhammadar Rasuulu llahi

Tafsiri:

Nashuhudia kuwa hapana mungu ila Allah na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah.

Shahada ndio kiingilio cha Uislamu. Yaani wasiokuwa Waislamu, wakiamua kuingia katika Uislamu, hukaribishwa na Waislamu kwa kutamkishwa hizi shahada mbili. Ukweli ni kwamba mtu hatakuwa Muislamu kwa kutamka tu haya maneno ya shahada bila ya kufahamu maana ya ndani.



Maana ya Shahada ya Kwanza:

“Nashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah”

Maana yake ni kwamba, huyu mja baada ya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia dalili mbali mbali zinazodhihiri katika umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, katika nafsi ya mwanaadamu, katika historia ya mwanaadamu, katika maisha ya Mitume na mafundisho yao, anayakinisha moyoni mwake kuwa yuko Mungu Muumba, Mpweke, Mwenye Uwezo juu ya kila kitu na Mmiliki wa kila kitu. Baada ya kuwa na yakini hii, huyu mja sasa anatoa ahadi kwa Allah(s.w) na kwa walimwengu wote kuwa, hatakuwa na mwingine yeyote atakaye muabudu au atakayemtii katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake kinyume na Allah (s.w).Kwa maana nyingine mja anayetoa shahada hii, anaahidi kuwa ataendesha maisha yake yote ndani ya mipaka aliyowekewa na Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii. Yaani wenye kumshuhudia Allah kikweli ni wale wanaofuata Uislamu katika kila kipengele cha maisha yao kama Allah (s.w) anavyowaamrisha katika aya zifuatazo:



“Enyi Mlioamini! Ingieni katika Uislamu wote (katika hukumu zote za Uislamu) wala msifuate nyayo za Shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui aliye dhahiri”. (2:208).



“Enyi m lioam ini! Mcheni Mw enyezi Mungu kam a ipasavyo kum cha; w ala msife isipokuwa mmekwishakuwa Waislamu kamili”. (3:102).



 

Maana ya Shahada ya Pili

“Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah”

Hii ndio sehemu ya pili ya shahada ambayo huikamilisha shahada ya kwanza. Labda swali litaulizwa: “Kumshuhudia Mtume Muhammad (s.a.w) kunakamilishaje shahada ya kwanza?” Tumeona kuwa maana halisi ya kumshuhudia Allah (s.w) ni kumuabudu Allah pekee katika kila kipengele cha maisha yetu.Tutamuabudu vipi Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yetu? Tutajuaje ni yepi aliyoyaharamisha Allah na yepi aliyoyahalalisha? Ni njia ipi tuifuate ili tupate radhi zake na ipi tuiepuke ili tuepukane na ghadhabu zake? Tutajuaje ipi njia sahihi na ipi potofu? Yote haya hatuwezi kuyajua mpaka tupate muongozo kutoka kwa Allah (s.w) mwenyewe.



Utaratibu aliouweka Allah (s.w) katika kuwaongoza wanaadamu ni kuwaleta Mitume miongoni mwa wanaadamu wanaume ambao huwaletea mwongozo na kuwafanya Waalimu wajuzi wenye hekima ili wawafundishe wanaadamu wenzao kinadharia na kimatendo juu ya Allah (s.w) na namna ya kumuabudu. Hivyo ili mja aweze kumjua Allah (s.w) na kumuamini ipasavyo na kisha aweze kumuabudu inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake, hanabudi kwanza kumuamini Mtume na kufuata mafundisho yake. Kwahiyo, sisi watu wa Umma huu wa Mtume wa mwisho, hatuwezi kuwa Waumini wa kweli wa Allah (s.w) bila ya kumshuhudia Mtume Muhammad (s.a.w) kuwa ni Mtume wa Allah (s.w).



Kumshuhudia Muhammad (s.a.w) kuwa ni Mtume wa Allah (s.w), ni kutoa ahadi kuwa utafuata mafundisho ya Mtume (s.a.w) vilivyo kwa kutekeleza yale yote aliyoyaamrisha na kuacha yale yote aliyoyakataza na kumuigiza mwenendo na tabia yake kama inavyosisitizwa katika Qur’an:

“Sema ( Muhammad kuwaambia watu): ‘Ikiwa nyinyi mnampenda Mw enyezi Mungu, basi nifuateni; (hapo)Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye Maghufira na Mwenye Rehema ”. (3:31)



“...Na anachokupeni Mtum e basi pokeeni na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na muogopeni Mw enyezi Mungu; kwa yakini Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu”. (59:7)



“Bila shaka mnao mfano mw ema kw a Mtume wa Mw enyezi Mungu kw a mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana ”. (33:21)

Kwahiyo, Muumini anapotoa shahada mbili anaahidi kwa dhati ya moyo wake kuwa atamtii Allah(s.w) na Mtume Muhammad (s.a.w) kwa unyenyekevu kwa kukiendea kila kipengele cha maisha ya kibinafsi na ya kijamii kwa mujibu wa mwongozo wa Qur-an na Sunnah ya Mtume (s.a.w). Mtu hatakuwa Muumini pale atakapoendesha maisha yake ya kibinafsi au ya kijamii kinyume na shahada kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo:



“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake w anapokata shauri,

w awe na hiari katika shauri lao. Na Mw enye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu uliowazi.” (33:36).



                   

Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3481

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Swala ya jamaa.
Swala ya jamaa.

Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.

Soma Zaidi...
maana ya Eda na aina zake
maana ya Eda na aina zake

Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.

Soma Zaidi...
Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu

Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?

Soma Zaidi...
Hadhi na haki za mwanamke katika jamii za Kigiriki hapo zamani
Hadhi na haki za mwanamke katika jamii za Kigiriki hapo zamani

(a) UgirikiTunajifunza katika historia ya Ulimwengu kuwa jamii ya Wagiriki ilikuwa miongoni mwa jamii zilizoanza kustarabika.

Soma Zaidi...
Hadathi ya kati na kati
Hadathi ya kati na kati

Posti hiibinakwenda kukufundisha kuhusu hadathi ya kati na kati.

Soma Zaidi...
Milki ya raslimali katika uislamu
Milki ya raslimali katika uislamu

Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.

Soma Zaidi...
Nini maana ya twahara katika uislamu
Nini maana ya twahara katika uislamu

Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo

Soma Zaidi...
Tarstibu za kulipa swaumu ya Ramadhani
Tarstibu za kulipa swaumu ya Ramadhani

Hapa utajifunza namna ambayo utatakiwa kulipa funga ya Ramadhani kwa siku ambazo hukufunga

Soma Zaidi...