picha

Madhara ya matusi katika jamii, na Kujiepusha na Matusi

15.

Madhara ya matusi katika jamii, na Kujiepusha na Matusi

15. Kujiepusha na Matusi


Mtu anayetukana ana lengo la kumdhalilisha mwingine. Waislamu tumekatazwa kutukanana na hata kuitana majina tusiyoyapenda kwa k ej eli.
“.... Wala msitukanane kwa kabila wala msiitane majina mabaya (ya kejeli). Jina baya kabisa kuitwa mtu ni “Fasiqi” baada ya kuwa yeye ni Muislamu. Na wasiotubu basi hao ndio madhalimu ”. (49:11)


Fasiq ni yule aliyebobea katika uasi. Yaani mtu anayejizatiti kumuasi Allah (s.w) kwa namna mbali mbali kama vile mwizi, mlevi,

mzinzi na kadhalika. Ni vibaya mno mbele ya Allah (s.w) kumsingizia au kumwita Muislamu ”mwizi” na huku si mwizi au kumwita “mnafiki” au “kafir” na huku ni Muislamu kamili. Tabia hii imekemewa vikali katika Qur-an:

“Kwa yakini wale wanaopenda uenee uovu kwa wale walioamini watapata adhabu iumizayo katika dunia na katika akhera, na Allah ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui”. (24:19).
Kutokana na makemeo haya, Muumini wa kweli hana budi kujiepusha na tabia ya kuwaita watu kwa majina mabaya kwani kufanya hivyo mtu hujilaani mwenyewe kiasi kwamba hayo majina mabaya yatamgeukia, kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Abu Dh-dhari(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana mtu atakayemsingizia mwingine uasi kwa Allah au akamwita “kafiri”, ila hayo yatamgeukia yeye mwenyewe iwapo huyo aliyemsingizia hayuko hivyo”. (Bukhari)



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 2655

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

sura ya 02

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Maswali juu ya hadithi

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya)

Soma Zaidi...
(viii)Wenye khushui katika swala

Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala.

Soma Zaidi...
Mawaidha Kutokwa kwa Shekhe

Karibu kwenye Darsa za mawaidha na Mafundisho ya dini.

Soma Zaidi...
Zingatio:

Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote.

Soma Zaidi...