16. Kuepuka Mabishano


Mabishano husababisha ugomvi, maudhi au kudharauliana. Mabishano yaweza kutibua mahusiano mzuri kati ya watu. Hivyo Uislamu unatukataza kubishana. Tunatakiwa tuzungumze na watu na kufahamishana mambo kwa hoja na sio kwa mabishano. Tunafundishwa katika Qur-an kuwa tukizungumza na watu ambao hawataki kuelewa bali wanafurahia ubishi tu, basi tusiendelee kuzungumza nao. Bali tuagane nao kwa salama.

“Na waja (wema) wa Rahman ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na wajinga wakisema nao, huwajibu “Salama ”. (25:63)