image

Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake

34.

Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake

34. Kuepuka Husuda



Husuda ni miongoni mwa magonjwa makubwa ya moyo. Mtu mwenye husuda anadonda la chuki moyoni mwake juu ya neema alizoneemeshwa mwingine na Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa maana nyingine anachukia utaratibu wa Mwenyezi Mungu (s.w) aliouweka katika kugawanya neema zake kwa waja wake. Hasidi kutokana na chuki yake dhidi ya mja aliyeneemeshwa na Mwenyezi Mungu (s.w), huwa tayari kwa hali na mali kumdhuru mja huyo asiye na hatia yoyote. Ni kwa msingi huu Mwenyezi Mungu (s.w) anatufundisha kujikinga kwake na shari za viumbe vyake, akiwemo hasidi kama tunavyosoma katika Suratul-Falaq:


Sema: Ninajikinga na Mola wa Ulimwengu wote. Na shari ya alivyoviumba. Na shari ya giza la usiku liingiapo na shari ya wale wanaopulizia mafundoni na shari ya hasidi anapohusudu(1 13:1-5)



Husuda husababishwa na kutotosheka na kutoridhika na neema za Mwenyezi Mungu (s.w). Hasidi anataka kila neema aliyotunukiwa mwingine awe nayo yeye au mwingine abakie bila neema hiyo. Anataka awe juu ya mwingine na aonekane wa maana pekee katika jamii. Akihisi kuwa kuna yeyote aliyemzidi kwa cheo, utajiri, elimu, watoto,umaarufu, hupandwa na moto wa chuki moyoni mwake ambao humsukuma kufanya visa mbali mbali dhidi ya huyo anayemhisi kuwa amemzidi au yuko sawa n aye. Muislamu anatakiwa ajitakase na uovu huu wa husuda kwa kutosheka na kile alichonacho akijua kuwa kila neema aliyopewa mwanaadamu imekadiriwa na Mwenyezi Mungu (s.w). Na hapana yeyote mwenye uwezo wa kupunguza neema ya mtu aliyokadiriwa na Mola wake hata kwa kiasi cha chembe ndogo iliyoje na hakuna yeyote awezaye kumuongezea mtu neema kuliko vile alivyokadiriwa na Mwenyezi Mungu


(s.w).
Pia Muislamu wa kweli anajitahidi kujiepusha na husuda ili asije akaziunguza amali zake njema alizozitanguliza na akawa miongoni mwa watakaohasirika katika maisha ya akhera.



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Kuweni waangalifu juu ya husuda, kwani husuda inaunguza amali njema za mtu kama moto unavyounguza kuni. (Abu Daud).



Husuda au wivu unaoruhusiwa ni ule unaofanywa kwa ajili ya kushindana katika kufanya mema. Wivu wa namna hii sio ule wa kuchukia kuwa kwa nini fulani ameneemeshwa bali ni ule unaomfanya mja ajitahidi zaidi kufanya mema kama anavyofanya au kumzidi mwingine. Mtume (s.a.w) ametufahamisha ni husuda ya namna gani inayoruhusiwa kwa Muislamu katika Hadithi ifuatayo:



Ibn Mas ’ud (r.a) am ehadithia kuw a Mtume w a Mw enyezi Mungu am esem a: Hapana husuda (inayoruhusiwa katika Uislamu) ila kwa watu wawili: “Mtu ambaye Mwenyezi Mungu (s.w) amempa mali na akampa uwezo wa kuitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu na mtu ambaye Mwenyezi Mungu amempa elimu na hekima akawa anafundisha wengine pamoja na yeye mwenyewe kuingiza elimu hiyo katika vitendo”. (Bukhari na Muslim)




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2228


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Uhakiki wa hadithi za mtume
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

nini maana ya Unafiki na sifa za unafiki katika quran na sunnah
Mnafiki ni yule anayeukubali Uislamu mdomoni (kwa kauli tu) lakini moyoni mwake na katika matendo yake anaukanusha. Soma Zaidi...

KULA HALALI NA ZILICHO KIZURI NI AMRI KATIKA UISLAMU
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "إنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إلَّا طَي... Soma Zaidi...

Husaidia wenye matatizo katika jam ii
Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran
Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Soma Zaidi...

Husimamisha swala
Husimamisha swala katika maisha yao yote. Soma Zaidi...

DARSA LA KUJIFUNZA KUHUSU QURAN NA SUNNAH
Soma Zaidi...

madhara ya kusengenya, na namna ya kuepuna usengenyaji
13. Soma Zaidi...

kuwa mwenye huruma na faida zake
25. Soma Zaidi...

Faida za kuwa na Huruma Kwenye Uislamu
23. Soma Zaidi...

quran na sayansi
QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Soma Zaidi...

Kujiepusha na Chuki na Uadui
26. Soma Zaidi...