12. Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana


Maongezi au mazungumzo yasiyo na maana ni yale yasiyoleta manufaa au kheri yoyote ila hasara tu. Mazungumzo haya yapo katika kupiga soga, kupiga porojo, kupiga hadithi za pauka pakawa, kutaniana, kubishana, na mengine ya namna hiyo. Mara zote mazungumzo ya aina hii huwapelekea watu kusengenya, kusema uwongo, kufitinisha, kugombana na kupoteza muda. Aidha mazungumzo ya aina hii huwasahaulisha watu kumkumbuka Allah (s.w).
Muumini hana budi kujiepusha na tabia hii ya kujiingiza kwenye mazungumzo ya upuuzi. Miongoni mwa sifa za waumini ni pamoja na kujiepusha na mambo ya upuuzi kama tunavyojifunza katika Quran:


“Hakika wamefuzu Waumini. Ambao katika Sw ala zao ni wanyenyekevu. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi”. (23:1-3).
Waja wema mbele ya Allah ni pamoja:

“Na wale ambao hawashuhudii uwongo na wanapopita penye upuuzi hupita kwa heshima (zao). (25:72).
Muislamu anashauriwa daima abaki kimya kama hana la maana la kuzungumza. Mtume (s.a.w) ametuusia:
“Kuwa kimya. Hii ni njia ya kumfukuza shetani na kuimarisha dini yako” (Ahm ad).

“Anayekuwa kimya (anayenyamaza wakati hana la maana la kuzungumza) atakuw a salama ”. (Ahmad, tirmidh).
“Ni jambo bora mno kwa Muumini kuacha yasiyomhusu” (Ma lik, Ahm ad, Tirm idh).
“Ni katika ubora wa Imani ya mtu kwa kuacha kujihusisha na mambo ya upuuzi”. (Tirm idh).