11.
11. Kuwa na Kauli Njema
Muislamu anatakiwa kila mara azungumze mambo ya maana na ya kheri. Ulimi utumike kusema ukweli, kuamrisha mema, kukataza maovu, kuwashauri wengine juu ya mambo ya kheri, kupatanisha waliogombana, kumsabihi Allah, kutoa elimu yenye kunufaisha watu na katika mazungumzo mengine ya kheri.
โNa ni nani asemaye kauli bora kuliko (yule) aitaye (watu) kwa Allah na (mwenyewe) akafanya vitendo vizuri na kusema (kwa maneno yake na vitendo vyake): โHakika mimi ni miongoni mw a Waislamu โ. (41:33).
Allah (s.w) anatuamrisha kusema maneno mazuri katika aya ifu atayo:
โNa waambie waja wangu waseme daima maneno yaliyo mazuri. Maana Shetani huchochea ugomvi baina yao. Hakika shetani kwa wanaadamu ni adui aliye dhahiriโ. (17:53)
Hivyo Muislamu hana budi kuzungumza na watu kwa maneno mazuri ya heshima. Maneno mazuri ya heshima yanajenga na kuzidisha upendo kati ya watu. Maneno mazuri ya heshima ni ngao ya kumzuilia shetani asiingilie kati na kuleta migongano na kutoelewana. Ni katika msingi huu tunaamrishwa tuulinganie Uislamu kwa hekima na kwa mawaidha mazuri:
โWalinganie (watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha m em a, na ujadiliane nao kw a namna iliyo bora. Hakika Mola w ako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake naye ndiye anayewajua walioongoka โ. (16:125).
Kauli njema ni yenye kumuongoza mja kwenda Peponi na kauli mbaya humuongoza mja kwenda Motoni kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Sahl bin Sa โd(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: โAtakayeweza kuchunga kilichopo kati kati ya taya zake (ulimi) na kilichopo katikati ya miguu yake miwili (utupu) ninaw eza kumhakikishia Pepo.โ (Bukhari).
Abu Hurairah(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: โMja atatamka neno lenye kumfurahisha Allah bila ya kuona uzito wake, bado Allah (s.w) humlipa malipo makubwa kutokana na neno hilo. Na mja atatamka neno lenye kumuudhi Allah bila ya kuona uzito wake, na bado linakuw a ndio mw anzo w a kumuingiza Motoni. (Bukhari).
Umeionaje Makala hii.. ?
Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao.
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukupa orodha ya dua 10 ambazo unaweza kuziomba kila siku.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูู ูู ุงููู ูุคูู ูููููู ุฃูู ูู ุนูุจูุฏู ุงูููููู ุนูุงุฆูุดูุฉู ุฑูุถููู ุงูููููู ุนูููููุงุ ููุงููุชู: ููุงูู: ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู "...
Soma Zaidi...Anapotajwa Mwenyezi Mungu au wanapokumbushwa juu ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hunyenyekea na kufuata kama walivyokumbushwa.
Soma Zaidi..."Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu, kama mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za ndugu zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za s
Soma Zaidi...