13. Kuepuka Usengenyaji


Kusengenya ni kumzungumza vibaya mtu asiyekuwapo hata kama hayo yanayozungumzwa juu yake ni kweli. Maana ya kusengenya imebainishwa vema katika Hadithi ifuatayo:


Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Wote mnajua kusengenya ni nini?” Walijibu, “Allah na Mtume wake ndio wajuzi zaidi”. Alisem a Mtum e: “Maongezi juu ya ndugu yako am bayo hayapendi” Aliulizwa Mtume, “Je, kama kile kinachozungumzwa ni kweli juu ya ndugu yangu ? ” Akasema (Mtume): “Kama hilo unalomsengenya kw alo analo, bado utakuwa umemsengenya na kama hilo unalomsengenya kw alo hanalo, utakuw a umemzulia ”. (Muslim)
Kama Muislamu anataka kuongea mabaya ya mtu angoje mwenyewe awepo na iwe kwa nia ya kumrekebisha na sio kwa nia ya kumuaibisha na kumfedhehesha. Ilipokuwa hapanabudi Mtume(s.a.w) aongee juu ya tabia mbaya ya mtu, alikuwa hamtaji muhusika moja kwa moja bali alikuwa akisema: “Wakoje watu hawa wanaofanya kadha wa kadha”.


Kusengenya hakuishii tu kwenye ulimi bali mtu aweza kusengenya kwa ishara ya macho, ulimi, midomo, mikono, miondoko na maandishi. Hata mwenye kusikiliza habari za kusengenya naye anahesabiwa kuwa amesengenya kama tunavyojifunza katika Hadithi:
Ibn ‘Umar(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Msikilizaji (wa maneno ya usengenyi) naye ni mmoja wa wasengenyaji”. (Tabrani).
Kusengenya ni miongoni mwa madhambi makubwa kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah. Katika Qur-an Allah (s.w) anatutahadharisha juu ya tabia ya usengenyi kama ifuatavyo:


“Adhabu kali itamthubutikia kila mlamba kisogo, msengenyaji. (104:1)

“Enyi mlioamini! Jiepusheni sana na dhana, kwani dhana ni dhambi. Wala msipeleleze (msipekue habari za watu). Wala baadhi yenu wasiwasengenye wengine. Je, mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? La! Hapendi. Na mcheni Allah. Bila shaka Allah ni mwenye kupokea toba na mwingi wa Kurehemu”.. (49:12).
Katika Hadithi kinabainishwa kina cha uovu wa kusengenya kama ifu atavyo:


Abdullah bin Mas ’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Kumsengenya Mu is lamu ni uovu na uasi na kumpiga ni ukafiri”. (Bukhari na Muslim).
Abdur-Rahmaani bin Ghanna(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Miongoni mwa waja wema mbele ya Allah ni yule au wale wanaomkumbuka Allah (kila wakati wanapokuwa macho) na miongoni mwa waja waovu mbele ya Allah ni wale wanaopita huku na huko wakiwateta (wakiwasengenya) watu ambao wanasababisha kutoelew ana kati ya w acha-Mungu ”. (Ahmad, Baihaqui).


Dhambi ya kusengenya ni miongoni mwa madhambi makubwa mbele ya Allah (s.w) yasiyosameheka mpaka kwanza asamehe yule aliyesengenywa kama tunavyojifunza katika Hadithi zifu atazo:


Abu Sayeed na Jabir(r.a) wamesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Kusengenya ni kubaya kuliko kuzini”. Wakauliza, “Ee Mtume wa Allah! Inakuw aje kusengenya kuw e kubaya kuliko kuzini? Alijibu Mtum e, “Mtu mwenye kuzini akitubia kwa Allah (s.w) anaweza kusamehewa, lakini msengenyaji hasamehewi mpaka kwanza asamehewe na yule aliyemsengenya ”. (Baihaqi).

Anas(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Msamaha kwa dhambi ya kusengenya hupatikana kwa kutakwa msamaha. kwa yule aliyesengenywa kwa kusema: “Ee Allah! Tusamehe pamoja naye”. (Ba ih aqi).
Kinachoruhusiwa katika Uislamu ni mtu kushitakia dhulma aliyofanyiwa na mtu kama inavyobainishwa katika Qur-an:

“Allah hapendi (watu) kutoa maneno ya kutangaza ubaya (kwa watu wengine) ila kwa yule mwenye kudhulumiwa, na Allah ndiye asikiaye ajuaye(4:148)
Pia tunaruhusiwa kueleza ubaya wa mtu kwa anayemuhusu ili amrekebishe. Tunaruhusiwa pia kumsema mtu kwa ubaya kwa lengo la kuwatahadharisha wengine na tabia mbaya ya mtu ili wasiathirike.