Zoezi - 1
1. Elimu ni nini?
2. “Sema, Je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?...” (39:9)
Ni kwasababu gani wanaojua hawawi sawa na wasiojuwa?
3. Unatoa maoni gani iwapo wanaojua na wasiojua wakawa sawa kiutendaji?
4. Toa maelezo yenye ushahidi wa Qur-an kuonyesha kuwa:
(a)Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa binaadamu na Mola wake.
(b)Kutafuta elimu ni amri ya kwanza kwa bin a adam u.
5. Onyesha kwa ushahidi wa Qur-an kuwa katika Uislamu mgawanyiko wa elimu katika “elimu ya dini” na “elimu ya dunia” haukubaliki.
6. “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.” (96:1) Kusoma kwa jina la Mola wako maana yake nini?
7. “.... Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu mambo aliyokuwa hayajui”. (96:3-5)
Orodhesha njia tano anazozitumia Allah (SW) katika kuwasiliana na wanaadamu.
8. Elimu yenye manufaa kwa binaadamu ni ile .................................
9. Eleza sababu tatu zinazopelekea elimu kupewa nafasi ya kwanza katika Uislamu.
*******************************
Umeionaje Makala hii.. ?
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Ibada yavfubga ni katika ibadavanbazo hufanya nakaribia dini zote kubwa. Ibada hii imekuwaikikabiliw na naswlo mengi.
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Maswali mbalimbali yanayohusu elimu ya dini ya kiislamu na mwongozo wa elimu na elimu mazingira.
Soma Zaidi...Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.
Soma Zaidi...QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh.
Soma Zaidi...