ndoto za kweli

(d) Ndoto za kweli



Njia nyingine ya kupata ujumbe kutoka kwa Allah ni njia ya ndoto za kweli. Historia inatuonyesha kuwa ndoto za Mitume daima zilikuwa zikitokea kweli; kwa hiyo ulikuwa ni ujumbe moja kwa moja kutoka kwa Allah (s.w). Ndio maana Nabii Ibrahim (a.s) alipoota kuwa anamchinja mwanawe, hakusita kutekeleza hilo kwa kuwa yeye na mtoto wake Ismail (a.s) walikuwa na uhakika kuwa ni amri kutoka kwa Allah kama inavyobaini katika Aya ifuatayo:


“… Ewe mwanangu! Hakika nimeona katika ndoto ya kwamba ninakuchinja. Basi fikiri, waonaje?” Akasema: “Ewe baba yangu! Fanya unayoamrishwa, utanikuta Insha-Allah miongoni mwa wanao subiri.” (37:102)
Kutokea kweli kwa ndoto ya Nabii Yusuf (a.s) kama inavyobainishwa katika Qur-an ni miongoni mwa ushahidi kuwa ndoto za Mitume ni ujumbe wa kweli na wa moja kwa moja (kama ndoto yen yewe ilivyo) kutoka kwa Allah (s.w). Hebu turejee kisa cha ndoto ya Nabii Yusuf (a.s) katika aya zifuatazo:


Kumbuka Yusuf alipomwambia baba yake: “Ewe baba yangu! Hakika nimeona katika ndoto nyota kumi na moja na jua na mwezi. Nimeviona vyote hivi vinanisujudia” (12:4)



Akasema (babaake): “Ewe mwanangu! Usiwasimulie ndoto yako (hii) nduguzo wasije wakakufanyia vitim bi (kwa ajili ya husda itakayow apanda). Hakika shetani kwa mw anaadam u ni adui aliye dhahiri (atawatia uchungu tu)”. (12:5)
Kutokea kweli kwa ndoto hii kunabainishwa katika aya ifuatayo:


(Na walipoingia kwa Yusuf), aliwainua wazazi wake na kuwaweka katika kiti (chake) cha ufalme. Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na (Yusuf) akasema: “Ewe babaangu! Hii ndiyo (tafsiri) hakika ya ndoto yangu ya zamani. Bila shaka Mola wangu ameihakikisha. Na amen ifanyia ihsani akanitoa gerezani na akakuleteni nyinyi kutoka jangwani; baada ya shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola w angu ni mw enye kulifikia alitakalo. Bila shaka yeye ni mjuzi na mwenye hikima”. (12:100).
Kutokea kweli kwa ndoto ya Mtume (s.a.w) kuwa Waislamu watangia Makka kuhiji kwa salama bila ya kuzuiliwa na mtu yeyote. Ndoto hii ilitokea kweli kama tunavyofahamishwa katika aya ifuatayo:



Kw a yakini Mw enyezi Mungu amemhakikishia Mtume wake ndoto yake ya haki. Bila shaka nyinyi mtaingia katika Msikiti Mtukufu Insha-Allah kwa salama; mkinyoa vichwa vyenu na mkipunguza nywele (kama ilivyowajibu kufanya hivyo wakati wa Hija). Hamtakuwa na khofu. Na (Mwenyezi Mungu) anajua msiyoyajua. Basi kabla ya haya atakupeni kushinda kuliko karibu. (48:27)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 677

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

quran na sayansi

2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.

Soma Zaidi...
Majina ya vijana wa pangoni

Makala hii inakwenda kukutajia majina ya vijana saba wa pangoni

Soma Zaidi...
MAADILI MEMA KATIKA UISLAMU

Yajuwe maadili mema yaliyotajwa katika quran

Soma Zaidi...
sura ya 02

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Husaidia wenye matatizo katika jam ii

Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada.

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa tabiina (wafuasi wa maswahaba)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...