Haya ndio yanayobatilisha Hija

Haya ndio yanayobatilisha Hija

Kubatilika kwa Hija
Hija itabatilika iwapo Haji ataacha kutekeleza moja wapo ya matendo yafuatayo:



(i) Ihram au nia ya Hija na kuwa katika hali ya Ihram ikiwa ni pamoja na vazi lake kwa wanaume na kuchunga masharti ya Ihram. Mtu akivunja masharti ya Ihram Hija haibatiliki lakini analazimika kufidia kwa kuchinja mnyama au kulisha maskini au kufunga. Ila kufanya tendo la ndoa ndani ya Ihram hubatilisha Hija kabisa.
Sa’i kati ya Safaa na Marwa.



(ii) Kuhudhuria katika uwanja wa Arafat siku ya mwezi 9 Dhul- Hija kati ya kuchomoza jua la mwezi 9 dhul-Hija na alfajir ya mwezi10 Dhul-Hija.



(iii) Tawaful Ifadha (Tawafu ya Nguzo).


Lengo la Hija
Kama tulivyojifunza katika masomo yaliyopita, lengo la ujumla la kuamrishwa kusimamisha nguzo tano za Uislamu, Shahada, kusimamisha Swala, Kutoa Zaka, Kufunga Ramadhani na Kuhiji Makka - ni kumuandaa mja aweze kuishi kulingana na lengo la kuumbwa kwake na kuletwa hapa duniani. Lengo la kuumbwa mwanaadamu limebainishwa katika Qur-an kuwa ni kumwabudu Allah(s.w.) katika kila kipengele cha maisha yake (Rejea Qur’an 51:56).



Ibada ya Hijja ni kilele au ni Chuo Kikuu cha kukamilisha maandalizi ya kumfikisha Muumini katika lengo la kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) katika kila kipengele cha maisha na kumuwezesha Muumini kuisimamisha dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa juu ya dini zote.



Namna Hija inavyomuandaa Muumini kuwa Khalifa waAllah katika jamii
Katika sehemu hii tutaangalia falsafa ya kila kitendo cha Ibada ya Hija kuanzia maandalizi ya safari mpaka mwisho wa safari na kuonesha namna ya kila kitendo cha Hijja kinavyomuandaa mja kuwa mcha-Mungu aliyetayari kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa hali na mali.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1762

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Hatua za kinga za ugumba na Utasa.

Ugumba ni “ugonjwa wa mfumo wa uzazi unaofafanuliwa kwa kushindwa kupata ujauzito baada ya miezi 12 au zaidi ya kujamiiana bila kinga mara kwa mara. Utasa  kutoweza kwa kiumbe hai kufanya uzazi wa ngono au kutoweza kupata mimba au kuchangia mimba.

Soma Zaidi...
Dua ya kuzuru makaburi, na utaratibu wa kuzuru makaburi

Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi.

Soma Zaidi...
Taasisi za Kifedha Katika Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu

- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n.

Soma Zaidi...
Fiqh.

Kipengele hichi tutajifunza chimbuko la fiqh na maana ya figh.

Soma Zaidi...
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu

Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...
Yaliyo haramu kwa mtu asiyekuwa na udhu

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ambauo ni haramu kwa mtu asiye na udhu.

Soma Zaidi...