Nguzo za imani

Nguzo za imani

Zifuatazo ni nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya dini ya kiislamu)

  1. Kumuamini Mwenyezi Mungu.
  2. Kuamini Malaika wake.
  3. Kuamini Vitabu Vyake.
  4. Kuamini Mitume Wake.
  5. Kuamini siku ya Mwisho.
  6. Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu.

  1. Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w).

-    Imani juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza kabisa kwa kila mwenye akili timamu kupitia ishara na maumbile mbali mbali yanayotuzunguka.

        Rejea Qur’an (3:190).

    -    Baada ya kumtambua, ni kumuabudu ipasavyo na kutomshirikisha katika sifa na majina yake matukufu na kiumbe yeyote.

        Rejea Qur’an (18:109), (31:27), (57:1-7), (59:22-24).

        Rejea Kitabu cha 2, EDK, Shule za Sekondari; Uk.8-16.

  1. Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu.

-    Malaika ni viumbe wa Mwenyezi Mungu walioumbwa kutokana na nuru kwa lengo la kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w).

-    Ni viumbe wa kiroho, wasio na jinsia, wenye mabawa na wenye uwezo wa kujimithilisha na kitu (kiumbe) chochote.

-    Hawana matashi ya kibinaadamu kama kula, kulala, kunywa, kuchoka, kuugua na hawana hiari kwa kila wanachoamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w).

    Rejea Qur’an (16:49-50), (7:206) na (21:26-27).

  1. Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).

-    Kuamini vitabu vya Allah (s.w) ni lazima kwa kila muumini wa kweli kama vilivyoainishwa katika Qur’an, ambavyo baadhi ni;

  1. Suhufi – aliyoteremshiwa Nabii Ibrahim (a.s) na Nabii Musa (a.s).
  2. Taurat – aliyoteremshiwa Nabii Musa (a.s)
  3. Zaburi – aliyoteremshiwa Nabii Daud (a.s)
  4. Injili – aliyoteremshiwa Nabii Isa (a.s) na 
  5. Qur’an – aliyoteremshiwa Nabii au Mtume Muhammad (s.a.w). 

-    Vitabu hivi vimeteremshwa kwa lengo la kuwaongoza wanaadamu katika njia sahihi na iliyonyooka ya maisha yao ili kufikia lengo la kuumbwa kwao.

    Rejea Qur’an (57:25) na (5:46).

Rejea Qur’an (6:92), (2:75), (4:14), (5:15), (5:48) na (16:64).

  1. Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).

-    Mitume ni wanaadamu wanaume walioteliwa ili kuwaongoza na kuwa mifano bora ya kuigwa kwa watu (ummah) wao katika kutekeleza ujumbe wao.

Rejea Qur’an (10:47), (6:83-86)

Rejea Kitabu cha 2, EDK, Shule za Sekondari; Uk.23.

  1. Kufahamisha na kufundisha juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w) na sifa zake. Qur’an (21:25), (16:36).
  2. Kufahamisha mambo ya ghaibu (Akhera) kama Moto, Pepo, Kiyama, Hisabu, Maisha ya Barzaq (kaburini) n.k. 
  3. Kufundisha njia sahihi ya maisha anayoiridhia Mwenyezi Mungu inayopelekea kunusurika na adhabu zake. Qur’an (3:164).
  4. Kusaidiana na wafuasi wao katika kuamrisha mema na kuondosha maovu katika jamii.
  5. Kuonya kutokana na adhabu na kubashiria mema kwa wafanyao mema.

  1. Kuamini Siku ya Mwisho.

-    Ni kuwa na yakini moyoni kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa.

    -  Kwa mujibu wa amali zao (vitendo vyao).

  1. Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu (s.w).

-    Amekiumba kila kiumbe kwa lengo maalumu na kukikadiria mahitaji yake yote.

    Rejea Qur’an (11:6), (57:22), (54:49) na (25:2). 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea

Umeionaje Makala hii.. ?

Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 3036

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu

Faradhi kwa maiti ya muislamu (edk form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab

Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa

Soma Zaidi...
Athari za kumuamini mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...