Uchumi Katika Uislamu
Maana ya Uchumi
- Ni uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa mali, rasilimali na huduma mbalimbali katika jamii ili kujenga mahusiano kati ya binaadamu na Allah (s.w).
Sifa za Uchumi wa Kiislamu
1. Dhana ya mafanikio
Huzingatia hatima yake ambayo ni kupata radhi za Allah (s.w) pekee.
2. Dhana ya umilikaji mali
Mmiliki hakika wa pekee wa mali na rasilimali zote ni Allah (s.w).
3. Dhana ya bidhaa
Ni kitu kilicho safi, kizuri, twahara, halali, n.k.
4. Dhana ya matumizi
Haifai kufuja au kutumia mali au rasilimali kwa njia za haramu.
5. Mizani ya wakati katika kutumia
Ni kujiuliza, nini matokeo ya mali au rasilimali hiyo baada ya muda fulani?
Njia na Misingi ya Uchumi Halali Katika Uislamu
i. Pasiwe na udanganyifu wowote katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa au mali.
Rejea Qurβan (17:35), (26:181-183), (83:1-4)
ii. Pasiwe na viapo katika kuuza au kununua bidha, kwani ni miongoni mwa kuuza kwa ujanja-ujanja.
Abu Qatada ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
βKuwa mwangalifu na viapo vingi katika uuzaji, kwa sababu japo
kunarahisisha uuzaji, kuna punguza barakaβ (Muslim).
iii. Pawe na uhuru kamili kwa mnunuzi kuikataa au kuikubali bidhaa baada ya kuiangalia.
iv. Bidhaa yenyewe iwe halali na iwe imechumwa kwa misingi ya halali pia.
v. Kuwepo na maelewano kati ya muuzaji na mnunuzi bila masharti. Dosari yeyote ya bidhaa ijulikane kabla ya manunuzi kufanyika.
vi. Muuzaji awe na uhuru wa kuuza bidhaa yake kwa bei yenye maslahi kwake na isiwe ya kumnyonya mnunuzi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi.
Soma Zaidi...kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah.
Soma Zaidi...Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu.
Soma Zaidi...