Taasisi za Kifedha Katika Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu

- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n.k.


- Benki hurahisisha kutoa huduma ya malipo kwa watu au wafanyakazi kupitia cheque, cash au hundi, n.k.

- Benki hurahisisha mtu kupata huduma ya malipo ya kifedha katika masafa ya mbali popote ulimwenguni kupitia matawi yake.

- Benki huepusha watu kuibiwa au kutembea na fedha nyingi au vitu vya thamani kubwa mkononi.

- Benki pia zinatoa mikopo mikubwa ili kuendeleza uchumi kwa watu na nchi kwa ujumla kama sekta za viwanda, kilimo, n.k.Benki za Kiislamu

Ni miongoni mwa taasisi za kifedha zinazotoa huduma katika msingi isiyokuwa na riba kupitia miradi au biashara zifuatazo;
i. Mudharabah

- Ni makubaliano kati ya watu wawili au zaidi ambapo mmoja hutoa mtaji na mwingine hushiriki kikamilifu kuendesha biashara au mradi.


ii. Musharakah

- Ni ushiriki kikamilifu wa watu wawili au zaidi katika kutoa mtaji na kuendesha biashara au mradi.


iii. Ijara – Uara wa Iktna

- Ni utaratibu wa kutumia fedha au mtaji kukodisha majumba, magari, mashamba, n.k. kwa ajili ya uzalishaji mali.


iv. Murabah
- Ni njia ya kununua bidhaa kwa wingi ili kuwauzia wafanyabiashara kwa
oda ya bei walioafikiana.

v. Muqaradhah

- Ni mtindo ambao mtu au benki hununua hisa “share” au “bonds” katika

kampuni za uzalishaji kwa makubaliano ya kugawana faida au hasara.Faida ya benki za Kiislamu

- Kuokoa uchumi wa jamii kutokana na riba na madhara yake.

- Hutoa mgawo na ushirika sawa katika kusimamia na kuendesha miradi na rasilimali kati ya maskini na wamiliki (matajiri).
- Huinua uchumi wa jamii kutokana na tahadhari na umakini mkubwa unaochukuliwa.