Muundo wa Dola ya Kiislamu
- Dola ni fani ya sayansi ya siasa yenye mamlaka ya juu ya kuamuru, kuongoza na kudhibiti vyote vilivyo ndani ya mipaka ya eneo, nchi yake.
- Serikali ndiyo taasisi kuu katika Dola ya Kiislamu yenye mgawanyo wa sehemu kuu tatu;
1. Bunge (Shura)
- Kutafsiri na kuweka utekelezaji wa sheria kutokana na Qur’an na
Sunnah.
- Kuainisha na kuidhinisha sheria, tafsiri au fat-wa mbali mbali kutokana na Ijma’a na Qiyaas.
- Kutoa fat-wa au hukumu za kidharura kutokana na hali ya siasa, uchumi, n.k.
2. Urasimu – Uulil’Amr (Adminstration)
- Ni wasimamizi wanaotakiwa kutiiwa katika utekelezaji wa maamrisho na makatazo mbali mbali ya Allah (s.w).
- Kuandaa jamii kupokea na kuyafanyia kazi maamrisho na makatazo yote ya Allah (s.w).
Rejea Qur’an (26:151-152)
3. Mahakama
- Kufafanua, kusimamia na kuhakikisha hukumu na sheria za Allah (s.w) zinatekelezwa ili kulinda haki, uadilifu na kuondoa uovu katika jamii. Rejea Qur’an (5:45-50)
? Uraia Katika Dola ya Kiislamu
- Kuna raia wa aina mbili
i. Waislamu – wote wazawa na wa kuhamia bila kuja tofauti za rangi, taifa,
n.k. wote ni ndugu wa moja. Qur’an (49:10), (8:72).
ii. Dhimmi – wananchi wote wasiokuwa waislamu katika Dola ya Kiislamu watakubaliwa tu iwapo watatii maamrisho ya Dola.
Msonge wa Uongozi Katika Dola ya Kiislamu
Msonge wa Uongozi Katika jamii ya
Kiislamu. Msonge wa Uongozi wa Dola ya Kiislamu
wakati wa Mtume (s.a.w)
1. Allah (s.w) – Qur’an 1. Allah (s.w)
2. Mtume (s.a.w) – Sunnah 2. Mtume Muhammad (s.a.w)
3. Majlis Shura – Bunge 3. Shura – (Sekretariati ya Mtume)
4. Viongozi wa ngazi mbali mbali 4. Viongozi wa Mikoa na wengine
5. Umma wa dola ya Kiislamu 5. Umma (Waislamu na wasio waislamu)
Sifa za Viongozi wa Kiislamu
i. Mjuzi wa Qur’an na Sunnah na kitengo cha anachoongoza.
ii. Mcha – Mungu
iii. Mwenye tabia njema
iv. Mwenye kujipamba na vipengele vya tabia njema. v. Mwenye afya au siha nzuri
vi. Aliyebaleghe.