3.
3.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu Kanuni kuu za uchumi katika Uislamu ni:
(i)Kumwamini Allah kuwa ndiye Muumba na mfalme wa ulimwengu huu yaani kumtii Allah katika mambo yote.
(ii)Binaadamu ni Khalifa wa Allah hapa duniani, hivyo wajibu wake ni kusimamisha amri ya Allah.
(iii)Ili kumsaidia mwanaadamu kutimiza wajibu wake kama Khalifa, Allah amemdhalilishia kila kitu katika ulimwengu huu:
“Mw enyezi Mungu ndiye aliyekutiishieni bahari ili humo zipite merikebu kwa amri yake ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru ”. (45:12).
“Je, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amevitiisha kwa ajili yenu vilivyomo ardhini…” (22:65)
“Je, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini na anakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? …” (31:20).
“Yeye ndiye aliyefanya ardhi iweze kutumika kwa ajili yenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika rizki zake na kwake ndiyo marejeo.” (67:15).
Hivyo kuzitumia neema hizo za Allah si dhambi bali ni katika kushukuru.
(iv)Kutokana na wajibu wa Ukhalifa wa Allah, mwanaadamu ataulizwa kwa neema alizompatia na atahesabiwa kwazo, ikiwa ni pamoja na namna alivyochuma na kutumia mali.
(v) Kuwa na mali au kutokuwa na mali nyingi au kidogo si dalili ya ubora au udhalili wa mtu. Hali zote mbili ni mtihani. Anachotazama Allah ni nyoyo za watu. Misingi au kanuni hizo zikithibiti katika moyo wa mtu zinakuwa na athari kubwa sana katika shughuli za kiuchumi za Muislamu.
Kanuni ya kwanza kwa mfano humfanya mtu afuate maamrisho ya Allah na hivyo atafanya kila njia ajiepushe na makatazo yake.
Pili, kwa kujua kuwa yeye ni Khalifa tu atajua yeye si mmilikaji wa hakika, hivyo atafuata maagizo ya huyo aliyempa ukhalifa yaani Allah.
Tatu, atajua kuwa utajiri si kitu cha kukipigania, bali mtu apiganie maisha bora na afya katika kutafuta radhi za Allah (s.w).
Nne, kwa kujua kuwa atahesabiwa na Allah anayeshuhudia kila kitu ataendesha shughuli zake za kiuchumi kwa kumcha Allah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu.
Soma Zaidi...Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria.
Soma Zaidi...Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu, masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike?
Soma Zaidi...