Haki ya kumiliki mali na mipaka yake katika uislamu

Je unaijuwa mipaka yako katika kumiliki mali. Ama unajuwa haki zako katika mali inayomiliki. Endelea na somo

Haki ya kumiliki mali

 


Kumiliki mali ni suala la kimaumbile na limeshikamana na silka ya kujihami (self presevation).Katika historia ya binaadamu suala la kumiliki mali limekuwa likiandamana na itikadi au falsafa inayotawala mahali.

 

Kwa mfano katika baadhi ya jamii za kitwaghuti umilikaji wa mali uko chini ya familia au huwa chini ya “watu wote” (mali ya umma) au huwa chini ya mtu au watu binafsi. Katika Uislamu kila kitu kipo chini ya miliki ya Mwenyezi Mungu:

 

“Sema Ee Mola uliyemiliki Ufalme wote! Humpa ufalme umtakaye na humuondolea ufalme umtakaye na humtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye, kheri imo mikononi mwako. Bila shaka wewe ni Mwenye Uwezo juu ya kila kitu ”. (3:26).

 


Hivyo ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mmilikaji wa hakika wa vitu vyote. Binaadamu anamiliki mali kwa dhamana tu siyo kwa hakika na kwa sababu hiyo ataulizwa jinsi alivyotumia. Katika Qur-an Allah (s.w) ameruhusu watu binafsi au kwa vikundi kumiliki mali pale aliposema:

 

“Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaom bee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe); na Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye.” (9:103)

 

Hivyo Uislamu unakubali na kuheshimu haki ya mtu au watu binafsi kumiliki mali.

 


Mipaka ya Umilikaji mali
(i)Mali hiyo iwe imechumwa kwa njia ya halali. Uislamu unaitambua haki ya kumiliki mali na haki ya kuilinda mali hiyo, lakini mali yenyewe iwe ya halali.

 


(ii)Mtu anaweza kuiuza au kuitumia mali yake apendavyo maadamu ana akili timamu. Iwapo hana akili timamu, itabidi apatikane mdhamini wa kuingalia mali hiyo kwa niaba na manufaa yake na manufaa ya jamii.

 


(iii)Maadamu mtu anayo mali basi anao pia wajibu wa kutekeleza majukumu yanayohusiana na mali aliyo nayo.

 


(iv)Uislamu unakataza ubakhili na israfu (ubadhirifu) katika matumizi. Mwenyezi Mungu anasema:

 

Wala usifanye mkono wako (kama) uliofungwa shingoni mwako, wala usikunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika. (17:29).

 

Enyi wanaadamu! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila sala; na kuleni (vizuri) na kunyw eni (vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Hakika Yeye hawapendi wapitao kiasi. (7:3 1).

 

Ubadhilifu ni kufanya mojawapo ya mambo matatu
Kwanza,
 kununua kitu usichokihitaji. Au kununua kitu unachokihitaji lakini kwa kiasi kingi kuliko unavyoweza kutumia. Kwa mfano kutengeneza chapati tano ilihali uwezo wako ni wa kula chapati mbili tu, halafu zile tatu ukazitupa jalalani.

 

Pili ni ubadhilifu kununua kitu chochote kile cha haramu, hata ikiwa kwa thamani ndogo namna gani. Kwa mfano hata kama masanduku laki moja ya bia yanauzwa kwa shilingi hamsini ukiitoa shilingi hamsini hiyo kununua pombe hiyo unaandikiwa madhambi ya ubadhilifu.

 

Tatu kutoa sadaka kwa ajili ya kujionesha kwa watu, badala ya kuandikiwa thawabu unaandikiwa madhambi ya israfu.

 


(v) Uislamu unakataza rasilimali zilizo katika jamii kuachwa bila kutumiwa Mtume (s.a.w) amesema mtu akiendeleza ardhi ana haki ya kuimiliki. Lakini akiiwacha kwa miaka mitatu bila kuitumia mtu mwingine ana haki ya kuiendeleza na kuimiliki.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1919

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)

Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume

Soma Zaidi...
Haki za binadamu kwa ujumla (basic human rights)

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu

Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.

Soma Zaidi...
Adhabu ya mzinifu katika jamii ya kiislamu

(iii) Adhabu ya UzinifuKatika Sheria ya Kiislamu mtu haadhibiwi mpaka atende kwa uwazi matendo yenye kuvuruga utaratibu na amani ya jamii.

Soma Zaidi...
Umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu

Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu

Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume.

Soma Zaidi...
Nadharia ya uchumi wa kiislamu

Dhana ya uchumi wa kiislamu imejegwa jui ya ukati na kati. Dhana hii imetofautiana sana na dhana nyinginezo kama ubepari na ujamaa.

Soma Zaidi...
Nini maana ya funga na ni lipi lengo lake

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la funga na maana yake katika uislamu.

Soma Zaidi...