Hekma katika hukumu za mirathi katika uislamu, na ni kwa nini wanaume wanazidi katika kurithi katika uislamu

Umuhimu na Hekima ya Sheria ya Mirathi ya Kiislamu

1. Mrithi na Mrithishaji mkuu ni Allah (s.w).

Rejea Qur’an (7:128), (57:10)2. Sheria ya Kiislamu kuhusu mirathi imezingatia nguzo kubwa ya jamii ambayo ni familia.


3. Mirathi katika Uislamu inahusika tu kwa ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu kinasaba wenye sifa za kurithi.


4. Kila mwenye sifa za kurithi, ana fungu lake lililokadiriwa kwa madhumuni ya ustawi wa jamii na kujenga mapenzi ya familia.


5. Uislamu umezingatia uhusiano wa karibu na wa mbali wa kinasaba na marehemu ili kila mmoja apate haki na fungu lake analostahili.


6. Mgawo wa mirathi katika Uislamu unazingatia uwiano wa nafasi na majukumu ya kila mwenye fungu ndani ya jamii.


7. Sheria ya Uislamu juu ya kurithi, inazuia kila aina ya upendeleo, dhuluma, unyanyasaji, n.k miongoni mwa warithi.
Hekima ya Mtoto wa Kiume Kupata Mara Mbili ya Mtoto wa Kike

1. Mtoto wa kiume ndiye mwenye majukumu makubwa ya kulea na kuhudumia familia na jamii kwa ujumla.


2. Mtoto wa kiume pia anajukumu la kuwa walii kwa dada zake pindi inapoidhinishwa kwa nafasi hiyo katika kuwaozesha.


3. Mtoto wa kike ikitokea ameachwa (ametalikiwa), kaka yake ndiye muwajibikaji wa kumtunza mpaka atakapoondoka katika himaya yake.

4. Mtoto wa kike pamoja na kuwa na majukumu machache kulinganisha na wa kiume, bado anafursa ya kupata fungu la mahari yake pia.


5. Mtoto wa kike pamoja na kuwa na fursa ya kumiliki mali na rasilimali, bado hana wajibu wowote wa kutuzimia kuhudumia familia ila kwa dharura.
Udhaifu wa Sheria za Kitwaghuti za Kurithi

- Katika jamii za kijahili, wanawake hawana haki na nafasi ya kurithi chochote.

- Katika zama za Jahiliyah, kabla ya kuja Mtume (s.a.w), sio tu wanawake walikuwa hawarithi, bali wao wenyewe walikuwa wanarithiwa kama mali pia.


- Sheria za kitwaghuti juu ya mirathi zimejengeka katika misingi ya upendeleo, dhuluma, unyanyasaji, n.k.


- Sheria za kitwaghuti hazizingatii sifa na vigezo vya warithi kwa marehemu kinasaba ambapo wasiostahiki wanaweza kupewa na wanaostahiki wakakosa.


- Hakuna mafungu maalum ya kurithi katika sheria ya kitwaghuti, bali kwa vigezo vya kijinsia.


- Sheria za kitwaghuti hazizingatii majukumu ya warithi.

Mfano mwanamke hupewa fungu kubwa kuliko mwanaume kwa kigezo kuwa eti hana uwezo wa kuchuma.


- Sheria za kitwaghuti huzingatia, hali ya maisha, uwezo kati ya warithi badala ya ukaribu wa nasaba na vigezo.