image

Misingi na Maadili Katika Uislamu

5.

Misingi na Maadili Katika Uislamu

MFUMO WA JAMII YA KIISLAMU

5.1. Misingi na Maadili Katika Uislamu

Maana ya Maadili

Ni mwenendo na tabia inayomfikisha mwanaadamu katika hadhi yake yak ukhalifa na kufikia lengo la kuumbwa kwake.


Mtazamo wa Makafiri juu ya Maadili

Wanafalsafa wa kikafiri wamejaribu kutoa majibu ya maswali ya msingi yafuatayo;

1) Ni lipi lengo kuu la maisha?

2) Ni zipi chem.-chem tunazozitegemea kutambua yapi mema na yapi maovu?

3) Nani msimamizi wa maadili katika jamii?

4) Ni kipi kichocheo kinachowafanya watu katika jamii wawe na maadili?Udhaifu wa majibu ya maswali haya

1) Lengo kuu la maisha hapa duniani ni;

1. Kuishi maisha yenye furaha – Je, ni furaha ya nini, ya aina gani, ya nani?

2. Kufikia utimilifu – Je, ni upi utimilifu?, wa nini? wa nani?, na kivipi?

3. Kutimiza wajibu kwa lengo la kutimiza wajibu – Je, ni lipi hilo lengo?, nani kaliweka?, lina maana gani?
2) Utambuzi wa mema na maovu ni;

1. Kwa kutumia uzoefu (human experience) – Je, ni uzoefu wa nani? wa nini?

Na kwa muda gani?

2. Kwa kutumia silka zetu (intuition) – Je, tutegemee akili ya nani? kizazi kipi?

3. Kwa kufikiri na kuhoji (rationalism) – Je, ni fikira zipi na za nani?3) Msimamizi wa maadili ni;

1. Kuwa yatasimamiwa na lengo husika – Je, lengo lipi ndio sahihi? n.k.

2. Kanuni zinazooana na hoja, akili (law of practical reason) – Je, ni akili ya nani itumike? Na kivipi?
3. Serikali kwa kutumia vyombo vyake.

4. Maoni ya watu katika jamii – social pressure4) Motisha wa Kufuata maadili ni;

1. Kutaka malipo na kuepuka adhabu (reward and punishment) – Je, ni nani anayetoa malipo au adhabu?
2. Maumbile ya binaadamu kutii na kuheshimu sheria.Hivyo, ni wazi kuwa majibu na hoja zote zinaudhaifu mkubwa sana na kamwe haziwezi kumwongozo mwanadamu kimaadili.


Mtazamo wa Uislamu juu ya Maadili

Udhaifu wa majibu ya makafiri juu ya maadili ni kutojua chanzo, hadhi na lengo halisi la mwanaadamu hapa ulimwenguni.
Hivyo, Uislamu unajenga maadili kwa kujibu maswali yafuatayo kwa usahihi;

1) Nini chanzo cha binaadamu? – Ni Allah (s.w)

Rejea Qur’an (15:28-29)2) Ni ipi hadhi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni? – Ni Khalifa, kiongozi wa

Allah (s.w). Qur’an (2:30-34).3) Ni lipi lengo kuu la maisha ya mwanaadamu na vyote vinavyomzunguka?

- Mwanaadamu ameumbwa ili kumuabudu Allah (s.w). Qur’an (51:56).

- Viumbe vinavyomzunguka ni kumwezesha binaadamu kufikia lengo lake.

Rejea Qur’an (2:29), (17:70)

4) Ni ipi chem chem ya ujuzi wa mema na maovu?

- Ni Allah (s.w) kupitia Vitabu vyake na Mitume wake. Qur’an (57:25)

- Qur’an na Sunnah (Hadith za Mtume (s.a.w))5) Ni nani msimamizi wa maadili katika?

- Ni imani thabiti juu ya Allah (s.w), siku ya mwisho na nguzo za imani.

Rejea Qur’an (33:36)

- Mamlaka na Dola ya Kiislamu.

Rejea Qur’an (22:41)

6) Ni kipi kichocheo cha watu Kufuata maadili katika jamii?

- Ni kuhofu adhabu ya Allah (s.w) duniani na akhera

Rejea Qur’an (89:25-26)

- Kutarajia msamaha na malipo ya pepo maisha ya akhera.

Qur’an (9:111), (61:10-13)

- Kuhofu mamlaka ya Dola ya Kiislamu.

                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 568


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Namna ya kuhiji, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Soma Zaidi...

Taratibu za mirathi katika zama za ujahilia
Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi. Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swala ya tahajud na swala za usiku yaani qiyamu layl
Post hii itakujuza jinsi ya kiswali swala ya tahajudi. Pia utajifunza jinsi ya kuswali swala za usikubyaanibqiyamublayl Soma Zaidi...

namna ya kuswali 6
Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu. Soma Zaidi...

Tofauti kati ya zakat na sadaqat
Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maana ya shahada
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Taratibu za kuchaguwa mchumba katika uislamu
Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

kanunu na sheria za biashara katika islamu
Soma Zaidi...

Ni yapi masharti ya Udhu na kujitwaharisha
Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya ndoa ya mke zaidi ya mmoja
Je jamii inachukuliaje swala la kuoa mke zaidi ya mmoja. Soma Zaidi...