Malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele.

Malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele.

Posti hii inahusu zaidi malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele zake, ni sababu ambazo upelekea kumsafisha mgonjwa nywele kama tutakavyoona hapo chini.

Malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele.

1.Kwanza kabisa tunamsafisha Mgonjwa nywele ili kuondoa wadudu kama vile chawa na mba.

Tunafanya hivyo kwa wakati mwingine kunakuwepo na chawa au mba ambao uweza kumsumbua mgonjwa na kufanya hali yake iweze kuwa mbaya kwa sababu chawa wanafyonza damu kama mgonjwa amelala kwa mda wa mwezi mmoja na hakuna usafi tunaona kuwa ni hatari kwa mgonjwa na pengine anahisi maumivu na hawezi kujikuna na hali hii usababisha hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

 

2. Tunafanyia mgonjwa usafi wa nywele ili kuweza kuruhusu vizuri mzunguko wa damu.

Kwa kufanya hivyo mzunguko wa damu inaweza kwenda vizuri kwa sababu kama kuna mba  kwa mda mrefu na sehemu hiyo mzunguko wa damu utakuwa shida kwa hiyo tunapaswa kusafisha sehemu hiyo ili kuweza kuruhusu mzunguko wa damu uenda vizuri.

 

3. Tunamsafisha Mgonjwa nywele ili kuweza kumfanya awe safi na kuweza kumpatia ahueni ya ugonjwa na anakuwa na matumizi mazuri na kujisikia vizuri kwamba anapendwa na kuna Watu wanamjali na pia mwonekano wa mgonjwa unakuwa vizuri.

 

4.Kwa hiyo tunapaswa kuwafanyia wagonjwa wetu usafi wa nywele kwa sababu kwenye nywele kunakuwepo na uchafu mwingi ambao Mgonjwa kama hajiwezi anashindwa kuomba masada ila mkijiongeza mkamsafisha anajisikia vizuri na anaweza kupata nafuu kwa sababu ya usafi mnaomuonyesha kwa hiyo tuwajali wagonjwa wetu hasa wanapokuwa hawajiwezi kwa kuwafanyia usafi kwa sababu na yenyewe ni sehemu ya tiba

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 2644

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 web hosting     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe

Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana.

Soma Zaidi...
Vyakula vya fati na mafuta

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya fati na mafuta

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa aliyepatwa na presha ya kushuka

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kushuka

Soma Zaidi...
Faida za chanjo

Posti hii inahusu zaidi faida ya chanjo, tunajua wazi kuwa chanjo Ina faida kubwa kwenye mwili wa binadamu na vile vile kwenye jamii kama tutakavyoona hapo chini.

Soma Zaidi...
Madhara ya kuchelewa kutibu tatizo la kiafya

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea endapo tatizo halijatibiwa.

Soma Zaidi...
Ratiba ya chanjo ya kifua kikuu

Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kifua kikuu, hiii ni ratiba ambayo chanjo hii utolewa na ushauri mbalimbali utolewa ili kuweza kufanikisha kazi ya chanjo hii

Soma Zaidi...