Ni zipi funga za suna, na faida na fadhila zake pamoja na wakati wake wa kufunga

Ni zipi funga za suna, na faida na fadhila zake pamoja na wakati wake wa kufunga

Funga za SunnahFunga za Sunnah tutakazoziorodhesha hapa ni zile alizozitekeleza Mtume (s.a.w) na kuzikokoteza. Umuhimu wa kutekeleza funga za Sunnah ni sawa na umuhimu wa kutekeleza Swala za Sunnah na Ibada nyinginezo alizoziagiza na kuzitekeleza Mtume (s.a.w) mbali na zile Ibada za faradh. Tunawajibika kutekeleza hizi Ibada za Sunnah kwa sababu zifu atazo:(1)Tunawajibika kumtii Mtume kwa kufuata yale aliyotuagiza na kuacha yale aliyotukataza na tunawajibika pia kumfanya kiigizo chetu.
(2)Ibada za Sunnah zinakamilisha zile Ibada za faradh zilizotekelezwa kwa upungufu kutokana na udhaifu wa kibinaadamu. Hivyo zinamuwezesha Muumini kufikia kwa uhakika lengo la kila ibada maalum -Shahada, Swala, Zakat, Swaumu, n.k.
Ni Karaha Kufunga Mwezi Mzima isipokuwa katika Ramadhani tu .Mtume (s.a.w), mbali na Mwezi wa Ramadhani, hakuonekana kufunga mwezi mzima mfululizo; bali katika mwezi wa Shaabani alionekana akifunga siku nyingi zaidi kuliko katika miezi mingine yote kwa kuwa ndio wa kujiandaa kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani. Pia Mtume (s.a.w) hakuonekana kuacha kufunga kabisa katika mwezi wowote ule kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:Aysha (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa akifunga (katika mwezi wa Shaabani) mfululizo mpaka tuseme hatafungua tena na aliacha kufunga mfululizo mpaka tuseme hatafunga tena; na sikumuona Mtume wa Allah akifunga mwezi mzima ila mwezi wa Ramadhani na sikumuona akifunga katika mw ezi mw ingine zaidi kuliko alivyokuw a akifunga katika mwezi wa Shaabani' (Muslim).(i) Kufunga siku tatu katika mweziMtume (s.a.w) ametukataza kufunga mfululizo na badala yake tufunge siku tatu kwa mwezi kwani kufanya hivyo mtu hupata ujira wa kufunga mwezi mmoja (jema moja hulipwa mara 10) kama inavyobainishwa katika Hadith ifuatayo:Abdullah bin Amr bin al-A as (r.a) amehadithia kuwa Mtume wa Allah alifahamishwa kuwa (Al-Aas) alikuwa akisimama katika swala usiku kucha na alikuwa anafunga kila siku katika maisha yake, ndipo Mtume wa Allah (s.a.w) akasema: 'Ni wewe uliyesema haya?' Nikamjibu: Ee Mjumbe wa Allah ni mimi niliyesema hayo. Ndipo Mtume (s.a.w) akasema: 'Huna uwezo wa kutosha kufanya hivyo. Funga na kufungua, lala na usimame kwa swala (usiku), na funga siku tatu katika mwezi: kwani


kila jema huzidishwa mara kumi, na huku ni kama kufunga maisha yote.' Nikasema (Al-Aas): Mjumbe wa Allah, nina uwezo wa kufanya zaidi ya hivi. Ndipo (Mtume) akasema: Funga siku moja na ufungue siku mbili zinazofuata.Nikasema: Mjumbe wa Allah nina uwezo wa kufanya zaidi ya hivyo. Mtume (s.a.w) akasema: Funga siku moja na ufungue siku inayofuata. Hiyo inajulikana kama funga ya Daud (a.s) na hiyo ni funga bora kuliko zote. Nikasema: Nina uwezo wa kufanya zaidi ya hivi. Hapa Mtume (s.a.w) akasema: 'Hakuna nyingine iliyo bora kuliko hii.' Abdullah bin Amr (r.a) anasema: 'Ningali kubali zile siku tatu (za kufunga katika mwezi) kama alivyonishauri Mtume wa Allah (s.a.w), zingalikuwa na thamani kw angu zaidi kuliko familia yangu na mali yangu.' (Muslim).Kutokana na Hadith hii, kufunga siku tatu katika kila mwezi pamoja na funga ya Ramadhani kunatosha kumpa mja mazoezi ya kumbakisha katika lengo la maisha yake na pia kumbakisha katika afya au siha ya kumuwezesha kutekeleza vizuri majukumu yake kwa jamii. Hata mtu mwenye uwezo wa kiafya kwa kiasi ambacho swaumu haiathiri majukumu yake kwa wengine, bado mtu haruhusiwi kufunga mfululizo. Mwisho wa wingi wa ufungaji ni ule wa funga ya Daud (a.s) kama ilivyobainishwa katika hadith hii. Hizi siku tatu katika mwezi si lazima zifungwe mfululizo na hapana siku maalum kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:Muazat bint Adyyah (r.a) ameeleza kuwa alimuuliza Aysha (r.a): 'Je, Mtume (s.a.w) alikuwa na tabia ya kufunga siku tatu katika kila mwezi?' Ndio, alijibu (Aysha). Nilimuuliza: 'Ni siku gani za mwezi alizokuwa anafunga ? ' Akasema: 'Hakuwa anajali ni siku gani ya mw ezi afunge.' (Muslim).Hata hivyo, kuzifunga mfululizo ni bora kwani Mtume (s.a.w)
alikuwa akifanya hivyo kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo: 'Abdullah bin Mas 'ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akifunga siku tatu za mwanzo za kila mwezi .... ' (Tirmidh, Nisai, Abu Da ud).Aysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume w a Allah aliw ahi kufunga Jumamosi, Jumapili na Jumatatu katika mwezi mmoja na Jumanne, Jumatano na Alhamisi katika mw ezi uliofuatia. (Tirmidh).Katika kufunga hizi siku tatu katika mwezi ni Sunnah kuzifunga siku za mbalamwezi kali - mwezi 13, 14, na 15 kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Abu Dharr(r.a) ameeleza kuw a Mtume wa Allah amesema; 'Ee Abu Dharr! Ukifunga siku tatu katika mwezi funga mwezi 13, 14, na 15'. (Tirmidh, Nis a i).

(ii)Funga za Jumatatu na AlhamisiNi Sunnah kufunga siku ya Jumatatu na Alhamisi kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuw a Mtume (s.a.w) alikuw a akifunga siku ya Jumatatu na Alhamisi. Akaulizwa:'Ee Mtume wa Allah! Unafunga siku ya Jumatatu na Alhamisi? Akajibu: 'Siku ya Jumatatu na Alhamisi Allah (s.w) humsamehe kila Mu is lamu ila w aw ili waliosusiana, Anasema Allah (s.w): 'Waache mpaka wapatane' (Ahmad, Ibn Majah).Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Amali zinawasilishwa siku ya Jumatatu na Alhamisi: Kwa hiyo ninapenda amali zangu ziwasilishwe wakati nimefunga'. (Tirmidh).Abu Qatadah(r.a) ameeleza kuw a Mtume (s.a.w) aliulizwa juu ya funga ya Jumatatu: Mtume alijibu: 'Nilizaliwa siku hiyo na nilianza kushushiwa wahay (Qur-an) siku hiyo.' (Muslim).Hadith hii inatufahamisha wazi kuwa Mtume (s.a.w) alisherehekea siku ya kuzaliwa kwa kufunga kila Jumatatu badala ya kusoma Maulid mara moja kwa mwaka.(iii)Kufunga siku sita katika Mwezi wa ShawwalKufunga siku sita katika mwezi wa Shawwal (Mfungo Mosi) ni sunnah iliyokokotezwa kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Abu Ayyub Al-Answaar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Atakayefunga Ramadhani kisha akafuatisha na funga ya siku sita katika mwezi wa Shawwal atakuwa kama amefunga mwaka mzima. ' (Muslim).Ilivyo ni kwamba, Allah (s.w), kwa huruma yake ameahidi kuwalipa waja wake wema mara kumi kwa kila jema watakalolifanya kwa ajili yake. Hivyo malipo ya kufunga siku 30 za mwezi wa Ramadhani ni sawa na malipo ya mwenye kufunga siku 300 (30 x 10) na malipo ya kufunga siku 6 za Shawwal ni sawa na mtu aliyefunga siku 60 (6 x 10). Mwaka mmoja una siku 360 (mwaka wa muandamo). Kwa hiyo utaona wazi kuwa mtu akifunga Ramadhani na kufuatisha siku sita za Shawwal malipo yake mbele ya Allah (s.w) ni sawa na mtu aliyefunga mwaka mzima.Je, hizi siku sita ni lazima zifungwe mfululizo kuanzia mwezi 2 Shawwal au mtu anaweza kufunga wakati wowote katika mwezi huu na bila kufululiza? Hili ni swali wanalojiuliza wengi. Wanavyuoni wametofautiana katika kujibu swali hili. Kwa mfano, Imamu Shafii, anaona kuwa ni vyema kufunga mfululizo kuanzia, mwezi wa pili Shawwal.Kwa upande mwingine Imamu Abu Hanifa anaona ni vyema kutozifunga mfululizo na kuzifunga wakati wowote katika mwezi huu wa Shawwal ili watu wasije kuichukulia kuwa kufunga mfululizo ni lazima na bila ya kufanya hivyo ibada hiyo haikamiliki.(iv)Funga ya ArafaArafa ni siku ya mwezi 9 Dhul-Hajj siku ambayo mahujaji husimama katika uwanja wa Arafa. Ni sunnah kwa Waislamu wengine kufunga ili kujihusisha kiroho na kisimamo cha Arafa. Katika Hadith iliyosimuliwa na Abu Qatadah (r.a) Mtume (s.a.w) amesema:'Funga katika siku ya Arafa hufuta dhambi (ndogo) za mwaka uliopita na mwaka ujao na funga ya Ashura inafuta dhambi za mwaka uliopita '. (Muslim).
Kwa Mahujaji ni vyema kutofunga katika siku ya Arafa. Mtume (s.a.w) hakufunga siku ya Arafa wakati alipohiji. Pia ni Sunnah kufunga katika kumi la mwanzo la mwezi wa Dhul-Hijjah (yaani kuanzia mwezi 1-9 Dhul-Hijjah. Tunajifunza hili katika Hadith ifuatayo:Hafsah (r.a) ameeleza kuwa kuna mambo manne ambayo Mtume (s.a.w) hakuyaacha kuyafanya - Kufunga siku ya Ashura, kufunga siku 10 za Dhul-Hijah, kufunga siku tatu kila mwezi na kuswali rakaa mbili ya swala ya Alfajir (Nisai).(v)Funga ya AshuraSiku ya Ashura ni siku ya mwezi 10 Muharram (mfungo nne) Mtume (s.a.w) kabla ya kufaradhishwa Ramadhani alianza kuwaamrisha Waislamu kufunga siku ya Ashura. Siku ya Ashura ndio siku ambayo Nabii Musa (a.s) na Banii Israil waliokolewa na Allah (s.w) kutokana na udhalimu wa Firaun na utawala wake kama tunavyojifunza katika Hadith ifu atayo:


'Ibn Abbas (r.a.) ameeleza kuwa, Mtume (s.a.w.) alipofika Madina aliwakuta Mayahudi wamefunga siku ya Ashura. Ndipo Mtume (s.a.w.) akawauliza: 'Ni siku gani hii ambayo mnafunga?' Walijibu: 'Hii ni siku kubwa (siku kuu) ambayo Allah (s.w.) alimuokoa Musa (a.s.) na watu wake na kumzamisha Fir'aun na watu wake. Musa (a.s.) akawa anafunga katika siku hii kama njia ya kuonyesha shukrani zake kwa Allah (s.w.) na sisi tunafanya hivyo vile vile'. Kisha Mtume wa Allah akasema: 'sisi tuwakweli zaidi na tuko karibu zaidi na Musa (a.s.) kuliko nyinyi. Hivyo Mtume (s.a.w.) alifunga siku hiyo na akawaamrisha Waislamu wafunge '. (Bukhari na Muslim)Umuhimu wa kufunga siku ya Ashura unabainika katika Hadith ifu atayo:'Abu Hurairah (r.a.) ameeleza kuwa Mtume wa Allah (s.a.w.) amesema: 'Funga bora kuliko zote baada ya Ramadhani ni funga ya mwezi wa Allah - Muharram, na swala bora kuliko zote baada ya swala za faradhi ni swala ya usiku (Tahajud)'. (Muslim)(vi) Funga katika mwezi wa ShaabanKatika Hadith tuliyoinukuu mwanzoni, tumejifunza kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akifunga kwa wingi katika mwezi wa Shaaban kuliko katika miezi mingine yote mbali na Ramadhan. Alipoulizwa kwa nini alipendelea kufunga sana katika mwezi huu, alijibu kuwa alikuwa akijiandaa kwa funga ya Ramadhani.
Pia tunajifunza katika hadith ifuatayo kuwa kufunga katikati ya mwezi wa Shaaban ni sunnah iliyokokotezwa:Imraan bin Husain(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) alimuuliza mtu mmoja:'Ulifunga funga yoyote katikati ya mwezi huu (Shaaban)?' Akajibu: Hapana'. Ndipo Mtume wa Allah akamwambia: 'Funga siku mbili (badala ya moja) baada ya kumaliza Ram adhani.'
                   
Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1810


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu
1. Soma Zaidi...

kanunu na sheria za biashara katika islamu
Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)
(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a. Soma Zaidi...

quran na tajwid
TAJWID Utangulizi wa elimu ya Tajwid YALIYOMO SURA YA 01 . Soma Zaidi...

Dalili (Alama) za Qiyama
Soma Zaidi...

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir
Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu. Soma Zaidi...

SIRI YA KIFO INAFICHUKA
Soma Zaidi...

Namna ya kuhiji, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

'Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye'
Soma Zaidi...

Kujiepusha na maringo na majivuno
Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri. Soma Zaidi...

Twahara na namna ya kujitwaharisha, nguzo zake na sunna zake
Soma Zaidi...