Kujitwaharisha Kutokana na Najisi
Kutokana na uzito wa kujitwaharisha tutazigawanya najisi katika makundi matatu
(a)Najisi ndogo.
(b)Najisi kubwa na
(c)Najisi hafifu
(a)Najisi Ndogo.
Najisi Ndogo
Inahusu najisi zote isipokuwa najisi ya mbwa na nguruwe. Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi ndogo ni kuosha paliponajisika kwa maji safi mpaka iondoke rangi na harufu ya najisi.
Kama tunatumia maji machache ambayo huharibika mara tu yatakapoingiwa na japo najisi ndogo, hatuna budi kutumia kata au chombo kingine cha kuchotea maji na kujitwaharisha pembeni kwa kujimiminia maji kupitia sehemu ile yenye najisi mpaka najisi hiyo iondoke.
Katika hali ya kawaida, maji safi hutumika kwa kustanjia. Tunazitwaharisha sehemu zetu za siri kwa mkono wa kushoto mpaka tuhakikishe kuwa najisi imeondoka. Katika hali ya dharura ya kukosa maji au ugonjwa usioruhusu kutumia maji, tunaruhusiwa kustanji kwa kutumia vitu vikavu kama vile karatasi laini (toilet paper), mawe, n.k. Tukistanji kwa vitu vikavu, kama vile mawe makavu tutapangusa sehemu zetu za siri kwa mawe matatu. Kama najisi ingalipo, tutaongeza mawe mawili mawili mpaka turidhike kuwa najisi imeondoka.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe jamii inachukuliaje swala la kuoa mke zaidi ya mmoja.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Katika uislamu hakuna sheria ya mwanamke kuingizwa eda na kutolewa eda kama ilivyozoeleka. Endelea na post hii ujifunze zaidi
Soma Zaidi...Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Haki ya KutalikiKatika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee.
Soma Zaidi...