picha

nguzo za uislamu: Kutoa zaka, lengo la kutoa zaka na faida zake

Kutoa Zakat.

nguzo za uislamu: Kutoa zaka, lengo la kutoa zaka na faida zake

NGUZO YA TATU YA UISLAMA: KUTOA ZAKA

Kutoa Zakat.
Umuhimu wa Zakat na Sadakat katika Uislamu.
i.Zakat ni nguzo ya tatu ya Uislamu.
Baada ya shahada mbili na kusimamisha swala nguzo muhimu sana katika uislamu ni kutoa zakat kama ilivyoainishwa katika hadithi.

ii.Kutoa zakat na Sadaka ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Kutoa zaka na vile tulivyoruzukiwa katika mali na huduma au misaada mbali mbali ni wajibu kwa waislamu wanaovimudu.
Rejea Qur’an (14:31) na (2:254).

iii.Kutoa Zakat ndio kitambulisho cha Uislamu na Ucha-Mungu wa mtu.
Muislamu akiacha au kukataa kutoa zakat kwa makusudi ni ishara ya kuritadi na kutoka katika Uislamu.
Rejea Qur’an (9:11) na (2:2-3).

iv.Kutoa Zakat na sadaka ni sababu ya mtu kufaulu Duniani na Akhera.
Miongoni mwa sifa za waumini na wacha-Mungu ni kutoa katika vile walivyoruzukiwa na muumba wao.
Rejea Qur’an (2:2-3), (23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).

v.Kutotoa Zakat na Sadaka ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.
Kutotoa katika vile tulivyoruzukiwa hupelekea mtu kustahiki adhabu hapa Duniani na Akhera pia.
Rejea Qur’an (9:34-35), (92:8-10) na (3:180).

Namna lengo la zakat linavyofikiwa.
Zakat na sadaka zinalengo la kutakasa mali na nafsi ya mtoaji na mpokeaji kama ifuatavyo;
i.Zakat na sadaka inavyotakasa mali ya mtoaji.
Zakat hutolewa 2.5% ya mali na kuwapa wanaostahiki, hivyo kuitakasa mali ya mtoaji kutokana na chumo la haramu na haki za watu.

ii.Zakat na sadaka zinavyotakasa nafsi ya mtoaji.
Utoaji mali kwa wanaostahiki huitakasa nafsi ya mtoaji kutokana na ubakhili, kuabudu mali, kibri, n.k katika kumiliki mali na kuwa na upole, huruma, n.k.
Rejea Qur’an (61:10-12) na (9:102-103).

iii.Zakat na sadaka inavyotakasa nafsi ya mpokeaji.
Utoaji wa zaka na sadaka kwa wanaostahiki huondoa chuki, husuda, uadui, unyonge kwa wasionacho na kuleta udugu, upendo, shukurani na ushirikiano.
Rejea Qur’an (9:60).

iv.Zakat na sadakat huitakasa jamii ya waislamu.
Utoaji wa zakat na sadaka hujenga jamii yenye udugu wa kweli, kujenga uchumi wa halali na kuondoa chuki na uadui baina ya masikini na matajiri.
Rejea Qur’an (61:4).


Kwa nini lengo la Zakat na Sadaka halifikiwi katika jamii yetu?
Pamoja na zakat na sadaka kutolewa na baadhi ya waislamu lakini malengo yake hayafikiwi, zifuatazo ni baadhi ya sababu;
i.Wengi watoao zakat na sadakat hawajui lengo lake halisi.
Waislamu wengi wanatoa zaka na sadaka kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio utakaso.

ii.Waislamu wengi hawatoi zakat kabisa.
Waislamu wengi licha ya kuwa na mali na uwezo wa kutoa zakat na sadaka lakini hawatekelezi au kuhimiza wengine katika kutoa mali zao pia.
Rejea Qur’an (2:2-3).

iii.Wengi watoao zakat na sadakat hawatekelezi masharti ya utoaji.
Pamoja na matajiri wachache kutoa zakat na sadaka, lakini bado hutoa kwa ria, masimbulizi, adha na kuleta uadui na fitna katika jamii.
Rejea Qur’an (2:264).

iv.Zakat na sadaka haikusanywi na kugawanywa kijamii.
Utoaji na ugawaji wa zakat na sadaka umekuwa unafanywa kila mtu kivyake, bila mpango maalumu wa kukusanya na kugawa kwa wanaostahiki.

v.Wengi watoao zakat na sadakat chumo lao ni la haramu.
Ingawa waislamu wengi hutoa zakat na sadaka, lakini lengo na matunda yake hayafikiwi kutokana na chumo lao kuwa haramu.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 4259

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 web hosting    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika

Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu.

Soma Zaidi...
Lengo la hijjah na matendo ya ibada ya hijjah na mafunzo yatokanayo

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Utaratibu wa kuzuru makaburi na dua zinazosomwa wakati wa kuzuru kaburi

Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika katika kuzuru kaburi la muislamu.

Soma Zaidi...
Sura zinazosomwa katika Swala ya Dhuha

Swala ya Dhuha ni swala ya sunna inayosaliwa wakati wa asubuhi baada ya jua kuchomoza na kupanda angalau kiasi cha mkuki (takribani dakika 15 baada ya jua kuchomoza) mpaka kabla ya adhuhuri. Ingawa hakuna sura maalum zilizowekwa kisheria, Mtume ﷺ alisoma baadhi ya sura zenye maana ya kuhimiza kheri na shukrani.

Soma Zaidi...
Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini?

Assalamu Alaykum Warahmatu-llah Wabarakaatuh Naomba kuuliza: Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini?

Soma Zaidi...