Posti hii inahusu njia za kumlisha Mgonjwa ambaye hawezi kujilisha wenyewe, hali hii uwa inawapata wagonjwa wale ambao hawawezi kujilisha wenyewe tunaweza kuwalisha kwa njia zifuatazo.
Njia za kuwalisha wagonjwa ambao hawawezi kujilisha mwenyewe.
1 Kwanza kabisa wagonjwa wengi wanashindwa kujilisha wenyewe kwa sababu mbalimbali labda hali zao haziwahusu kwa sababu ya aina ya ugonjwa kwa hiyo tunapaswa kuwalisha kwa sababu chakula na dawa vinaendana kwa hiyo Mgonjwa hasipokula hawezi kupona mapema kwa hiyo hata mgonjwa kama mgonjwa hawezi kujilisha anapaswa kulishwa kwa kufuata njia zifuatazo.
2. Mweke Mgonjwa kwenye hali ambayo ataweza kukaa vizuri na kula chakula na kama hajiwezi mwekee kitu cha kumfanya aweze kukaa vizuri na msafishe kinywa kabla ya kumpatia chakula kwa sababu kinywa kikiwa kisafi uongeza hamu ya kula.
3. Mwekee kitambaa kwenye kifua ili kuweza kumkinga na vyakula ambavyo vinaweza kudondokea nguo na pia leta sahani ya chakula karibu na mgonjwa na kumbuka kunawa mikono kabla ya kumlisha Mgonjwa na baada ya kumlisha Mgonjwa.
4. Kaa karibu na mgonjwa na pia ni vizuri kuwa na msaidizi wakati wa kumlisha Mgonjwa na chukua chakula cha mgonjwa na kiweke kwenye kijiko kuanzia kwenye mdomo wa kijiko na mlishe kidogo kidogo na wakati wa kumlisha subiri kwanza atafute ameze na ndipo umwekee chakula kingine .
5.Na pale Mgonjwa unapomlisha mruhusu kupumzika kidogo akimaliza kumeza na mlishe tena na akiwa amepumzika ongea naye taratibu na pia endelea kumlisha mpaka atakaposhiba na kama anahisi kichefuchefu mpumzishe kumlisha mpaka apo baadae atakapo tulia.
6. Mpatie maji ya kunywa au juise akimaliza kula mpe kidogo na kwa utaratibu mpaka atakapomaliza kiasi ulichompimia na akimaliza msafishe mdomoni ili kutoa mabaki yaliyobaki na pia mpanguse chakula ambacho kilianguka kwenye nguo.
7.Kwa hiyo jamii nzima inapaswa kuchukua wajibu wa kuwalisha wagonjwa kwa sababu wagonjwa walio mahututi wengi ufariki mapema kwa kukosa chakula sio kwamba chakula hakipo hapana ila njia na elimu kuhusu kuwalisha wagonjwa hawana kwa hiyo natumaini tutaweza kuwatisha wagonjwa wetu baada ya kujua haya
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
makala hii inakwenda kukupa faida, kazi na athari za vitamini B mwilini. Nini hutokea endapo utakuwa na upungufu wa vitamini B mwilini?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi aina kuu za vidonda,kuna aina kuu tatu za vidonda ambapo kila aina utumiwa kwa njia yake kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mkojo wa kawaida kwa kila mwanadamu na unavyopaswakuwa, mkojo wa kawaida kwa binadamu huwa na sifa zifuatazo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna ya kumsafisha mgonjwa kinywa,ni njia unazopaswa kufuata wakati unamsafisha mgonjwa kinywa hasa wale walio mahututi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatua za kufuata unapohisi umeambukizwa na virus vya ukimwi. Kwa sababu watu wengi wanakuwa na kiwewe anapohisi ameambukizwa na virus vya ukimwi kwa hiyo wanapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi njia za kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa wa vidonda vya tumbo, ni njia ya kuwasaidia wagonjwa waliopata madonda ya tumbo
Soma Zaidi...Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...