Njia za kukabiliana na presha ya kupanda/hypertension
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kupanda
NJIA ZA KUKABILIANA NA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)
1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa dakika kama 30 mpaka 60. si lazima uwe unakimbia ama mazoezi magumu ya kutoa jasho, hapana unaweza hata kuamua kutembea kwa miguu kwa mwendo mrefu kwa lisaa limoja na ikawa ni mazoezi tosha.
2.Kula vyakula vilivyo bora kwa afya, ambavyo vinasaidia kupunguza ama kuzuia presha. Kitaalamu mlo huu huitwa DASH yaani Diet Aproaches to Stop Hypertension. Vyakula hivi ni kama:
A.Matunda
B.Mboga za majani
C.Nafaka nzima
D.Samaki, karanga na korosho
E.Wacha kula vyakula vyenye mafuta mengi
3.Punguza ulaji wa chumvi sana. Kuzidi kwa ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi kunaweza kusababisha presha ya kupanda. Kitaalamu ni kuwa ukila chumvi sana mwili unahitaji kupata maji mengi na hali hii itapelekea presha.
4.Punguza uzito uliozidi mwilini. Rafiki mkubwa wa presha ni kuzidi kwa uzito. Na tambuwa kuwa uzito wa mwili unatakiwa uendane na urefu wa mtu na si umri ama unene alio nao. hivyo tambua. Ili kuhakikisha kama uzito wako upo sawa unaeza kujipimia kiuno chako. Kikawaida wanaume wnatakiwa viuno vyao visizidi nchi 40 na wanawake viuno vyao visizidi nchi 35.
5.Punguza matumizi ya sigara ama wacha kabisa. Ndani ya sigara kuna kemikali za nicotine na nyinginezo. Nicotine ni rafiki sana na presha ya kupanda.
6.Punguza unywaji wa pombe ama wacha kabisa. Unywaji wa pombe sio hatari tu wa afya ya moyo lakini pia unaweza kuleta shida nyingine za kiafya kama saratani. Hakikisha kama ni mnywaji unapunguza unywaji ama unawacha kabisa itakuwa ni bora kwako.
7.Hakikisha huna misongo ya mawazo. Misongo ya mawazo inaweza kuwa ni adui mkubwa wa afya ya ubongo. Ni vyema kusamehe wanaokukosea na kuomba msamaha unapo kosea hali zote hizi mbili zitakusaidia kupunguza misongo ya mawazo. Jichanganye na watu na pemba kuwa mbali na fujo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 ai web app 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 web hosting 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Soma Zaidi...Msaada kwa wenye tonsils
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa wenye tonsils, kwa wale wenye tonsils wanapaswa kufanya yafuatayo ili kuweza kupambana na ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Vipi utaepuka maumivu ya kichwa ya mara kwa mara?
maumivu ya kichwa ni moja ya dalili za kiafya ambazo huashiria hali isiyo ya kawaida. hata hivyo maumivu ya kichwa yanaweza kutokea hata kama sio mgonjwa. Hapa nitakuletea sababu zinazopelekea kuumwa na kichwa mara kwa mara.Maumivu
Soma Zaidi...Mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe
Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana.
Soma Zaidi...Yajue malengo ya kusafisha vidonda.
Posti hii inahusu zaidi malengo ya kusafisha vidonda, kwa sababu Kuna watu wengine huwa wanajiuliza kwa nini nisafishe kidonda hospitalini au kwenye kituo chochote Cha afya, yafuatayo ni majibu ya kwa Nini nisafishe kidonda.
Soma Zaidi...Imani potofu juu ya ugonjwa wa Ukimwi.
Posti hii inahusu zaidi imani potofu juu ya ugonjwa wa Ukimwi,ni Imani walizonazo watu wengi kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi.
Soma Zaidi...