Namna ya kujikinga na kifua kikuu

Namna ya kujikinga na kifua kikuu

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia au kujikinga na kifua kikuu, hizi ni njia ambazo utumika ili kujikinga na kifua kikuu

Namna ya kujikinga na kifua kikuu.

1.Kwanza kabisa tunajua kua kifua kikuu kinaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kwa hiyo ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu tunapaswa kutumia njia ili kuepuka kusambaza ugonjwa huu ambao ni hatari kwenye jamii. Tuanaweza kujikinga kama ifuatavyo.

 

2.Tunapaswa kuwakinga kwanza watoto wakiwa wadogo kwa kuwapatia chanjo ya kuzuia kifua kikuu, hii chanjo utolewa kwa watoto pindi wanapozaliwa na utolewa kwenye mkono wa jua wa mtoto na tunapaswa kuhakikisha kuwa kovu limetokea kama halijatokea chanjo urudiwa, kwa hiyo njia ya kwanza ni kwa kutumia chanjo kwa watoto.

 

3.Kufunika mdomo wakati wa kupiga chafya.

Wakati wa kupiga chafya tunapaswa kufunika mdomo kwa leso safi ili kuepuka mate kusambaa kwenye sehemu mbalimbali wakati wa kupiga chafya na kunawa mikono pindi unapogusa mate au majimaji yoyote kutoka kwenye pua au mdomo.

 

4.Kuvaa Maski au barakoa unapohisi kama kuna mtu mwenye Maambukizi ya kifua kikuu au mtu mwenye Maambukizi ya kifua kikuu anapaswa kuvaa Maski ili kuepuka hali ya kuwaambukiza wengine na kufanya ugonjwa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

5.Kuepuka kutupa vitambaa au vitu vyote vilivyohusiana na kupanga makamasi vinapaswa kutupwa kwenye sehemu ya takataka ili kuepukana na kusambaa kwa ugonjwa wa kifua kikuu.

 

6.Pia tukumbuke kuwa mgonjwa wa kifua kikuu kama hajaanza dawa ndipo anaweza kusambaza ugonjwa ila kama akianza dawa na akazitumia kwa mda wa wiki mbili hawezi kuambukiza kwa hiyo tuachane na tabia za kuwanyanyapaa na kuwatenga wagonjwa wa kifua kikuu , maana ugonjwa huu unatibika na una dawa na wengi wamepona

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 4597

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Njia za kuingiza chanjo mwilini

Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Njia za kujilinda dhidi ya mapunye

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujilinda dhidi ya mapunye

Soma Zaidi...
Namna ya kutoa huduma ya kwanza

Huduma ya kwanza ni huduma anayopewa mgonjwa au mtu yeyote aliyepata ajali kabla ya kumpeleka hospitalini

Soma Zaidi...
Athari za mkojo mwilini.

Posti hii inahusu zaidi athari za mkojo mwilini, kwa kawaida tunafahamu kwamba mkojo ni matokeo ya mkusanyiko wa uchafu wa maji maji yanayokusanyika kutoka mwilini ikiwa mkojo umebaki mwilini usababisha madhara mbalimbali kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Kazi za vitamin B na makundi yake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take

Soma Zaidi...
Zijue kazi za Figo mwilini

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa Figo mwilini, Figo ni ogani ambayo kazi yake ni kuchuja sumu mwilini.

Soma Zaidi...