Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama anaenyonyesha
MWANAMKE MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI AKIWA MJAMZITO AMA ANAVYOVYESHA.
Watu wengi wamekuwa kijiuliza sana kuhusu hatma ya ujauzito kwa mwenye virusi vya ukimwi. Je ni kiasi gani mtoto aliye tumboni atakuwa salama?. ni tahadhari gani mjamzito mwenye virisi vya ukimwi achukuwe. Na atakapojifunguwa ni muda gani ataendelea kunyonyesha? Katika kipengele hiki tutaangalia kwa ufupi habari hii kama ifuatavyo:-
1.Je inawezekana kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kupata HIV/UKIMWI?Yes inawezekana, na hili ni swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Itambulike kuwa kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika si lazima kuwa nawe utaathirika, ila kauli hii isieleweke vibaya. Kwani njia ambayo inaongoza leo katika kueneza maambukizi ya HIV ni kushiriki tendo la ndio. Mtu anaweza kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kuathirika endapo:-
A.Endapo hakutatokea michubuko wakati wa tendoB.Endapo muathirika ametumia dawa za ART kwa muda mrefu kwa kufuata masharti hata viral load yake ikawa haionekani (undetected) na akadumu kwa hali hii walau miezi 6C.Endapo walitumia kinga wakati wa kushiriki tendo.
2.Je HIV ma UKIMWI hupelekea mimba kutoka?Inategemea, ila kwa ufupi HIV na UKIMWI huhatarisha ujauzito endapo muathirika hatakuwa mwangalifu ama hatafata maelekezo vyema. Wajawazito walioathirika inashauriwa wafike kituo cha afya mapema sananili kupatiwa maelekezo jinsi ya kulea mimba yake kwa usalama bila ya kuathiri afya ya ujauzito wake. Hata hivyo wanatakiwa wafuate maelekezo vyema.
3.Je maisha ya mtoto yapo hatarini endapo mama mjamzito ana HIV na UKIMWI?Ni kweli kama mama mjamzito hatakuwa makini, anaweza kuweka maisha ya mtoto wake hatarini. Na si maisha ya mtoto tu bali hata maisha yake pia.
4.Je mtoto anapataje HIV na UKIMWI kutoka kwa mama?A.Wakati wa kujifunguwa kama kuna kosa litafanyika.B.Wakati wa kumnyonyosha kuanzia miezi sita toka kuzaliwa mtotoC.Wakati wa kumlea kama mama hatakuwa makni
5.Kwa nyakati za sasa wajawazito wote wanatakiwa kuzalia kwenye kituo cha afya maalumu. Hii ni kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Hatahivyo wakunga wa jadi pia wamepatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya dharura. Ila inalazimika kwa mwenye HIV afanye juu chini azalie hospitali kwa usalama zaidi wa mtoto wake.
6.Je kunyonyesha mtoto kunawza kumuambukiza HIV?Yes inawezekana, hata hivyo mama akiwa makini na maelezo aliyopewa, katu hatoweza kumuambukiza mwanaye. Inashauiwa mtoto kunyonya kwa muda wa miezi 6 tu ama chini ya hapo. Ni kuwa endapo mtoto atakuwa na michubukomdomoni ama tumboni.
7.Mama asimchanganyie mtoto ziwa lake, maziwa ya kopo na chakula. Kama ataamuwakumnyonyesha ndani iwe ni ndani ya miezi 6 tu na asimpe chakula chochote. Na kama ameamuwa kumpa chakula asimnyonyeshe tena. Na kama ameamuwa kumpa maziwa ya makopo ampe hayo tu na asimnyonyeshe. Anaweza kuchanganya chakula na maziwa ya kopo ama ya ng’ombe na si yake na kitu chingine chochote. Mama awe makini sana na jambo hili, asimchanganyie mtoto maziwa yeke na kitu kingine chochote. Hali hii inaweza kusababisha michubuko mdomoni ama tumboni na kusababisha kupata maambukizi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi msaada au namna ya kuwahudumia wale wasioona hedhi na wamefikiwa kwenye umri wa kuweza kuona hedhi.
Soma Zaidi...Saratani ya matiti ji moja kati ya saratani zinazosumbuwa wqnawake wengi. Katika somo hili utajifunza chanzo cha kutokea saratani ya matiti
Soma Zaidi...Miongoni mwa matunda yenye virutubisho vingi ni pamoja na papai, nanasi, tikiti, palachichi, pera, karoti, hindi na boga. Lakini katika matunda haya yapo ambayo kwa mimba changa anatakiwa awe makini, kama papai na nanasi. Sasa vipi kuhusu mimba ya
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazosababisha kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Mdau anauliza ni muda gani mwanamke anaweza kujijuwa kuwa amepata ujauzito.
Soma Zaidi...dalili za ugonjwa wa tezi dume, na sababu za kutokea kwa tezi dume, maana ya tezi dume na athari zake
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukufundisha dalili za kujifunguwa, hatuwa za kujifunguwa na kuzalisha, pia utajifunza mabo muhimu kabla na wakatii wa kujifungua.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa harufu mbaya kwenye uke ukizingatia usafi huwa unafanyika mara kwa mara ila harufu bado inaendelea kuwa mbaya kwa hiyo tutaona sababu hapo chini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka.
Soma Zaidi...