Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu.
1. Kwanza kabisa unapaswa kuchuma mmea wako kwenye bustani Kama ulikuwa umepanda mwenyewe au ukinunua sokoni unashika majani Yako unayakata yanakuwa mafupi au wengine upenda kuyaacha hivyo hivyo yalivyo, unaandaa maji yako yaliyosafi unaosha vizuri sana kwa sababu kama yametoka sokoni hujui yameshikwa na wangapi au mmea ulikuwa kwenye mazingira yapi, unaosha vizuri na baadae unasuuza na maji safi .
2. Unaandaa maji safi kwenye sufuria na acha yachemke na yasichemke kwa mda mrefu na baadae ipua na acha upoe,au wakati mwingine una ponda ponda majani yaliyosafishwa vizuri unachemsha maji unatumbukiza kwenye maji yaliyochemka bila kuchemshwa na unafunika na mfuniko kwa mda na baadae ukipoa unafunua mfuniko.
3. Mchanganyiko wako ukipoa unatumia Kikombe kimoja kutwa mara tatu kwa siku thelathini na unatumia Kikombe cha Kawaida kisiwe kukkubwa sana au cha kati Ili mradi kiwe Kikombe cha kati na ukimaliza dozi Yako unaweza kutulia kwa mwezi mmoja na baadae ukaendelea nawaambia magonjwa ya saratani, uvimbe, nevu, homa utasikia kwenye taarifa ya habari, hayatatokea yakupate.
4. Kuna wengine wanatumia mchai chai kwa njia tofauti ambapo wanachukua majani ya mchai chai wanatumia kwenye chai kila siku badala ya kutumia majani na njia hiyo ni nzuri sana , hasa hasa usipoweks sukari au ukaweka kidogo ni vizuri kwa sababu na matumizi hayo ni sehemu ya tiba.
5. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuanza kutumia huduma hii ya mchai chai kwa sababu Haina gharama na jitahidi kupanda mwenyewe hata kama hauna sehemu chukua kopo upandepo yaani liwe kama ua kwenye Bustani Yako, natumain utapata afya njema kwa kutumia mmea huu aina ya mchai chai.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kupambana na saratani
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza faida na matumizi ya asali mwilini.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula korosho
Soma Zaidi...