Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.
Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo:
Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.Tunajifunza katika Qur-an kuwa jambo la kwanza alilotunukiwa Adam (a.s) mara tu baada ya kuumbwa kwake ni kupewa elimu.
“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote...” (2:3 1)
“Majina ya vitu vyote” katika aya hii inaashiria fani zote za elimu ambazo anahitajia mwanaadamu hapa duniani ili afikie kwa ufanisi lengo la kuumbwa kwake. Pia tunajifunza katika Quran kuwa mwenye elimu na hekima amepewa kheri nyingi.
(Mungu ) humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. (2.269).
Kutafuta elimu (kusoma) ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu. Tunajifunza kutokana na historia ya kushushwa Qur-an kuwa Wahay wa kwanza kumshukia Mtume (s.a.w) ambao ndio ulimtawazisha rasmi kuwa mtume ni ule unaopatikana katika aya tano za mwanzo za Suratul-’Alaq:
“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.Ambaye amemuumba mwanaadamu kwa ‘Alaq (kitu chenye kuning’inia). Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui”.(96:1-5)
Kutokana na aya hizi, kwa muhtasari, tunajifunza yafu atayo:
1. Kusoma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza waliloamrishwa wanaadamu na Mola wao.
2. Kusoma kwa jina la Mola wako ni kusoma kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu au ili kuweza kumwabudu Allah(s.w) inavyostahiki na kusimamisha Uislamu katika jamii.
3. Radhi za Mwenyezi Mungu zitapatikana pale mwanaadamu atakapoweza kufikia lengo la maisha yake la kumuabudu Allah (s.w) kwa kuzingatia maamrisho na mipaka ya Mwenyezi Mungu katika kila kipengele cha maisha.
4. Amri hii ya kusoma hailengi fani maalum tu ya elimu; bali kila fani itakayomuwezesha mwanaadamu kufikia lengo la maisha yake kwaufanisi.
5. Chanzo au chimbuko la fani zote za elimu ni Allah (s.w). Hivyo kwa Muislam mlango wa kwanza wa elimu ni kusoma kwa mazingatio Qur-an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) na kusoma maarifa ya Uislamu kwa ujumla kutokana na vyanzo hivi viwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Maswali juu ya Sunnah na hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mambo yaliyo sunnah siku za Idi ('iyd) siku ya sikukuu
Makala hii inaelezea mambo mbalimbali yaliyothibiti katika Sunnah kuhusu namna ya kuadhimisha siku ya ‘Iyd kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Miongoni mwa mambo hayo ni kuvaa mavazi mazuri, kula kabla ya Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr, kuleta Takbira, kuswali kwenye Muswallaa, pamoja na adabu nyingine zinazopaswa kufuatwa na Waislamu katika siku ya Sikukuu.
Soma Zaidi...