Hii ni hadithi ya pili katika kitabu cha Arbain Nawawiy
‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa mbele ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa ghafla akatutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua.
Alienda akakaa karibu na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Rasuli) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislaamu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Uislamu ni kukiri kuwa hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na Muhammad ni Rasuli wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga swawm Ramadhwaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.” (Akasema yule mtu yaani Jibriyl): “Umesema kweli.” Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Rasuli na kumsadikisha.
Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan. Akasema: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake na siku ya Qiyaamah, na kuamini Qadar (majaaliwa ya Allaah) ya kheri zake na shari zake.” (Akasema Jibriyl): “Umesema kweli.”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan.” Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.”
Akasema (Jibriyl): “Niambie kuhusu Qiyaamah.” Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji.” Kisha akamwambia: “Nijulishe alama zake.”: Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari.” Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari).
Kisha akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Rasuli wake wanajua zaidi. Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.” [Muslim]
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Post hii inakwenda kukugundisha adabu zinazotakikana kwa mwenye kuomba dua.
Soma Zaidi...Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini
Soma Zaidi...Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukupa orodha ya dua 10 ambazo unaweza kuziomba kila siku.
Soma Zaidi...Hapa utakwendabkuijuwabhistoria ya uandishi wa hadithi. Pia utaijuwa sababu iliyopelekea uandishi wa hadithi kuwa mdogo .
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha umuhimu wa nasaha katika dini
Soma Zaidi...Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihi (b) Hasan/Nzuri.
Soma Zaidi...