Kukubaliwa kwa dua kunategemea mahusiano yako na Allah. hata hivyo kuna baadhi ya mabo ukiyafanya dua yako inaweza kukubaliwa kwa haraka zaidi. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kuomba dua ikubaliwe.
Ili kuomba dua itakayokubaliwa unatakiwa uzingatie adabu za dua, nyakati za kuomba dua pia ujuwe hali zinazozunguruka dua yako. Hapa nitakueleza baadhi ya taratibu za kuomba dua itakayokubaliwa
Zingatia adabu na taratibu za dua kama ifuatavyo:-
1. Omba dua ukiwa twahara
2. Elekea kibla
3. kuwa twahara katika mavazi na mwili
4. Anza na kumsifu Allah (Tahmid, kwa kusema Alhamduliilahi rabbil-'alamiina)
5. Mswalie mtume (Swala ya mtume)
6. waombee dua waislamu wote
7.Taka istighfar kwa kusema Astaghfirullah (mara kadhaa)
8. sasa omba dua yako
Zingatia nyakati za kuomba dua. Nyakati zifatazo dua hukubaliwa rahisi:-
1. siku ya ujumaa
2. usiku wa manane
3. Baada ya Swala
4. Baada ya adhana
5. Wakati ukiwa umefunga
6. Wakati unapofanya jambo jema la kumfurahisha Allah
Pia omba Dua yako katika hali hizi:-
1. ukiwa umefunga
2. baada ya kusoma quran
3. Toa sadaka kisha muombe Allah dua yako
4. Mfanyie wema mtu aliye mbali akikuombea dua yake itakubaliwa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Post hii inakwenda kukufundisha namna ama staili ambazo Allah hujibu dua za watu.
Soma Zaidi...Nini kilichangia ongezeko la uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha ni nyakati zipi ambazo Allah hukubali dua kwa urahisi.
Soma Zaidi...