Kwa nini uislamu umeipa elimu nafasi ya kwanza

Elimu imepewa nafasi kubwa sana katika uislamu.

Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?


Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislam kwa sababu zifu atazo:
Kwanza, elimu ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kumtambua Mola wake vilivyo na kumuabudu ipasavyo kwa unyenyekevu kama Qur-an inavyothibitisha:

 


“... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalam (waliozama katika fani mbali mbali)” (35:28).

 

Pili, elimu iliyosomwa kwa mrengo wa Qur-an ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa Ulimwenguni. Khalifa ni mja anayetawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) kwa kufuata kanuni na sheria zake. Nabii Adam (a.s) aliwathibitishia Malaika kuwa ana uwezo wa kuutawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) baada ya kuelimishwa fani zote za elimu (majina ya vitu vyote) na kuahidiwa mwongozo kutoka kwa Allah (s.w).

 


Tatu, kutafuta elimu ni Ibada maalumu ya hali ya juu kuliko Ibada zote. Kwa mujibu wa Qur-an Swala ni Ibada maalumu ya hali ya juu na ni dhikri kubwa au zingatio kubwa juu ya Allah (s.w)

 

“… Hakika swala humzuilia (mja) na mambo machafu na maovu na ni dhikri kubwa kwa Allah (s.w)” (29:45).

 


Pia katika Hadith Mtume (s.a.w) amesisitiza: “Nguzo kubwa ya Dini (Uislamu) ni swala, mwenye kusimamisha swala kasimamisha Dini na mwenye kuacha sw ala kavunja Dini.”
Hivyo kwa mujibu wa Qur-an na Hadith sahihi za Mtume (s.a.w), swala ni Ibada yenye hadhi ya juu kuliko Ibada zote mbele ya Allah (s.w); lakini bado Ibada ya kutafuta elimu inachukuwa nafasi ya juu zaidi kuliko swala kwani swala haiwezi kusimama bila ya kuwa na ujuzi stahiki.
Nne, mwenye elimu ananafasi bora ya kumuabudu Mola wake inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake kama inavyosisitizwa katika Qur-an:

 

“... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu…” (35:28)
Pia Qur-an inasisitiza juu ya umuhimu wa elimu kwa kuuliza:

 

“… Je, waweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.” (39:9)
Kimsingi wanaojua wanatarajiwa wafanye mambo kwa ufanisi zaidi kuliko wasiojua. Kwa msingi huu Allah (s.w) anasisitiza tena katika aya ifuatayo:

 


“Mwenyezi Mungu ataw ainua (daraja) w ale w alioamini miongoni mwenu, na waliopewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda yote…” (58:11)
Hivyo, kutokana na aya hizi (35:28, 39:9 na 58:11) tunajifunza kuwa waumini wenye elimu wana daraja zaidi kuliko waumini wengine kwa sababu wanao uwezo zaidi wa kuona dalili za kuwepo Allah (s.w) na utukufu wake kwa undani zaidi, jambo ambalo huwapelekea kumuogopa Mola wao na kumuabudu inavyostahiki katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao kama inavyobainika katika aya zifuatazo:

 

“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonesha kuw epo Allah (s.w) kwa wenye akili. (3:190)

 

Ambao humkumbuka Mw enyezi Mungu w akiwa wima, wakiwa wamekaa na wakiwa wamelala. Na hufikiri (tena) umbo la mbingu na ardhi (wakasema) Mola wetu! Hukuviumba hivi burebure tu. Utukufu ni wako. Basi tuepushe na adhabu ya moto.” (3:190).
Pia kutokana na aya hizo tunajifunza kuwa waumini wenye elimu wanao uwezo mkubwa wa kufanya mambo kwa ufanisi jambo litakalowapelekea kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika jamii.

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1156

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.

Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini.

Soma Zaidi...
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir

Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu.

Soma Zaidi...
Mtazamo wa uislamu juu ya dini

Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini.

Soma Zaidi...
Sifa za wuamini zilizotajwa katika surat Al-ma'aarij

Kwa hakika binaadamu ameumbwa, hali ya kuwa mwenye pap atiko.

Soma Zaidi...
NGUZO ZA IMANI

Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s.

Soma Zaidi...