Wanapokujia wanafiki, husema: "Tunashuhudia ya kuwa kwa yakini wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Wanapokujia wanafiki, husema: "Tunashuhudia ya kuwa kwa yakini wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wake na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanafiki ni waongo, (wanasema wasiyoyasadiki). (63:1)
Wamevifanya viapo vyao ndizo ngao za kujikingia, wakajikinga na kupitishwa njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakifanya. Na hayo ni kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo muhuri umepigwa juu ya nyoyo zao; kwa hivyo hawafahamu lolote. Na unapowaona, miili yao inakupendeza, na kama wakisema, unasikiliza usemi wao (kwa vile unavyopendeza); lakini wao ni kama boriti zilizoegemezwa; (wamekaa magogo tu hapo, hawafahamu lolote); wanadhani kila kishindo (kinachozuka) ni juu yao, (ni cha kuwatafuta wao). Hao ni maadui, jihadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki! (63:2-4)
Na wanapoamabiwa: "Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu akuombeeni msamaha (kwa makosa yenu mliyoyafanya), huvigeuza vichwa vyao (kwa kuonyesha kuwa hawataki); na unawaona wanajizuia na wakijiona wakubwa. Ni sawa kwao ukiwatakia msamaha au usiwatakie msamaha, Mwenyezi Mungu hatawasamehe; hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu maasi (wenye kutoka katika taa yake). Hao ndio wanaosema: "Msitoe mali kwa ajili ya wale walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ili waondokelee mbali (hapa nchini kwetu, Madina)." Na hazina za mbingu na ardhi ni za Mwenyezi Mungu; lakini wanafiki hawafahamu.(63:5-7)
Wanasema: "Tukirudi Madina, Mwenye utukufu atamfukuza mnyonge." Na utukufu hasa ni wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wa Waislamu; lakini wanafiki hawajui. (63:8)
Sifa za wanafiki zilizoainishwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo:
(i) Wanasema wasiyoyasadikisha katika nyoyo zao. Katika aya ya kwanza (63:1), Allah (s.w) amewaita wanafiki waongo kwasababu, pamoja na kudai kuwa wanashuhudia kuwa Muhammad (s.a.w) ni Mtume wa Allah (s.w), wanamkanusha Mtume nyoyoni mwao na katika matendo yao. Hawakuwa tayari kuufuata Uislamu ule aliofundisha Mtume Muhammad (s.a.w).
(ii)Hufanya viapo vyao kuwa blanketi la kufichia maovu wanayoyafanya dhidi ya Uislamu na Waislamu.
(iii)Huonesha Uislamu wao katika mavazi na maneno, lakini katika utendaji wako mbali kabisa na Uislamu.
(iv)Huishi kwa wasiwasi wakikhofia kuwa uovu wao waliouficha utafichuliwa.
(v)Wanazuia watu wasitoe sadaqa zao kuusaidia Uislamu na Waislamu wanaostahiki kusaidiwa.
(vi)Hawako tayari kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa makosa yao.
(vii)Wanaendekeza ubaguzi wa kikabila/ na cha warangi
Kwa kuhitimisha sehemu hii ya "sifa za wanafiki" tumejifunza kuwa wanafiki ni wale watu wanaodai kuwa ni Waislamu, na ilihali vitendo vyao katika maisha ya kila siku ni kinyume kabisa na Uislamu.
"Na katika watu wako wasemao "Tumeamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na hali ya kuwa wao si wenye kuamini." (2:8)
Si wenye kamini kwa sababu tabia na mwenendo wao katika mchakato wa maisha yao kila siku katika ngazi ya binafsi na ya jam ii ni sawa na tabia na mwenendo wa makafiri wanaomkanusha Allah (s.w) na siku ya mwisho. Mnafiki hajiiti mnafiki wala hana alama yoyote katika mwili wake ya kuonesha unafiki wake, bali huwa mnafiki kutokana na tabia yake hata kama atadai kuwa ni Muislamu kwa mavazi, kuswali, Kufunga, kuhiji, n.k. Hivyo Muumini wa kweli hanabudi kuwa Muislamu mtendaji kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah na hanabudi kujiepusha na tabia zote za kinafiki. Waislamu huangukia kwenye unafiki kutokana na moja ya sababu tatu zifuatazo:
(i)Kutokuwa na Elimu sahihi juu ya Uislamu. Elimu sahihi ni ile inayomuwezesha mtu kujua lengo la kuwepo kwake hapa duniani na namna ya kulifikia.
(ii)Kupupia maisha ya dunia kwa dhana kuwa dunia ni sehemu ya starehe.
(iii)Khofu inayotokana na kuogopa kufa au kukabiliwa na magumu mbali mbali yanayosababishwa na maadui wa Uislamu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 676
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 kitabu cha Simulizi
Kujielimisha kwa Ajili ya Allah (s.w).
Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s. Soma Zaidi...
KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)
Soma Zaidi...
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Munaafiqun
Wanapokujia wanafiki, husema: "Tunashuhudia ya kuwa kwa yakini wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...
Kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini?
Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA
Soma Zaidi...
Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake
Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu. Soma Zaidi...
Kuamini Qadar ya Allah (s.w)
Soma Zaidi...
Maswali juu ya nguzo za Imani
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kwanini Uislamu Ndio Dini Pekee Inayostahiki Kufuatwa na Watu?
Soma Zaidi...
Muhtasari wa madili malezi ya jamii kama ilivyobainishwa katika Qur-an
(v)Kuwaombea dua wazazi. Soma Zaidi...
Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah
Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Soma Zaidi...
mafunzo ya TAWHID, maarifa na imani ya dini ya kiislamu
YALIYOMO1. Soma Zaidi...