image

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah

Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe).

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-TawbahMwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Kwa nini umewapa ruhusa ?(Ungengoja)mpaka wanaosema kweli wakupambanukie, na uwajue waongo(9:43).


Hawatakuomba ruhusa wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. (Hawatakutaka ruhusa) kutoipigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anawajua wanaomcha.(9:44)


Wanakuomba ruhusa wale wasiomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na nyoyo zao zina shaka; kwa hivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao. (9:45)


Na kama wangalitaka kutoka (kwenda vitani) bila shaka wangaliandalia maandalio yake (lakini hawakufanya lolote, ni alama kuwa hawakuwa na nia ya kwenda huko vitani). Mwenyezi Mungu hakupenda kutoka kwao (kwenda huko vitani). Na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa (na Shetani) "Kaeni pamoja na wanaokaa. "Kama wangalitoka pamoja nanyi wasingalikuzidishieni ila mchafuko, na wangekwenda huku na huku baina yenu kukutakieni fitina (kukugombanisheni).Na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza (watu wabaya hao). Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu. Tangu zamani walitaka kukutilieni chokochoko (na fitina) na wakakupindulia mambo chini juu, mpaka ikafika haki na kudhihirika amri ya Mwenyezi Mungu; juu ya kuchukia kwao. (9: 46-48)


Na miongoni mwao yuko anayesema (kumwambia Mtume): "Niruhusu (nisije vitani) wala usinitumbukize katika fitina (kwa kuona wanawake wa huko nikafitinika nao)." Hakika wao wamekwishatumbukia katika fitina. Na kwa yakini Jahannamu itawazunguka makafiri (wasiwe na pa kutokea). Ukikufikia wema (wewe Mtume na Masahaba) unawachukiza; na ukikufikia msiba husema: "Tuliangalia vizuri tangu zamani mambo yetu (kwa hivyo hatukufikwa na balaa hii)," na hugeuka wanakwenda zao nao wamefurahi. Sema: "Halitatusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ni Mola wetu." Basi Waislamu nawamtegemee Mwenyezi Mungu tu. (9:49-51)Sema: "Nyinyi hamtutazamii sisi ila (kupata) moja katika mema mawili (ima kushinda tukapata ngawira au kuuawa tukapata Pepo). Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake au (inayopatikana) kwa mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi." Sema: (kuwaambia hawa wanafiki): Toeni (mali yenu) kwa kupenda au kwa kutopenda, hakutakubaliwa kwenu (kutoa huko). Hakika nyinyi ni watu maasi. " Na haikuwazuilia ikubaliwe kwao michango yao, ila kwa sababu walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawafiki mahala pa kusali ila katika hali ya uvivu. (9:52-54)


Wala hawatoi (hivyo wanavyovitoa) ila kwa kuchukia. Yasikufurahishe mali yao wala watoto wao. Anataka Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa hayo katika maisha ya dunia, na zitoke roho zao, na hali ya kuwa ni makafiri. Na


wanaapa kwa (jina) la Mwenyezi Mungu kwamba wao ni pamoja nanyi. Wala wao si pamoja nanyi.Bali wao ni watu wanaoogopa (ndio maana wanasema uwongo huku kwa Waislamu na huko kwa makafiri). Kama wangalipata pa kukimbilia au mapango au mahali (pengine) pa kuingia, (bila shaka) wangekimbilia mbio huko, wanakwenda shoti (kama farasi waliochafuka). (9:55-5 7)


Na miongoni mwao (hao wanafiki) wako wanaokusema katika (kugawa kwako) sadaka. Wanapopewa katika hizo (Sadaka na Zaka) huridhika; na wakitopewa katika hayo wanakasirika. Na kama wangeyaridhia yale aliyowapa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na wakasema: "Anatutoshea Mwenyezi Mungu, karibuni Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila zake, na Mtume wake (pia); hakika sisi tunaelekea kwa Mwenyezi Mungu." (9:58-59)Sadaka hupewa (watu hawa): - Mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislamu) na katika kuwapa Uungwana watumwa na katika Kuwasaidia wenye madeni na katika mambo aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na katika (kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima. Na miongoni mwa (hao wanafiki) wako wanaomuudhi Mtume na kusema: "Yeye ni sikio tu" (yaani anasikia maneno bila ya kuyapima. Waongo wakubwa). Sema "Sikio la kheri kwenu "; anamuamini Mwenyezi Mungu na anawasadiki wanaoamini. Na ni rehema kwa wale wanaoamini miongoni mwenu. Na wanaomuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu inayoumiza (9:60-61)


Wanakuapieni Mwenyezi Mungu ili kukuridhisheni (japo wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume), hali ya kuwa Mwenyezi Mungu - na Mtume wake (pia) - ana haki zaidi ya kuwa wao wamridhishe, ikiwa wao ni wanaoamini. Je, hawajui ya kwamba anayeshindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi yeye atapata moto wa Jahannamu kukaa humo daima? Hivyo ndiyo hizaya kubwa (udhalilifu inayowangojea). (9:62 -63)Wanafiki wanaogopa kuteremshiwa sura itakayowatajia (unafiki wao) uliomo katika nyoyo zao. Sema: "Fanyeni tu mzaha, hakika Mwenyezi Mungu atayatoa nje hayo mnayoyaogopa." Na kama ukiwauliza (kwa nini waifanyia mzaha dini) wanasema: "Sisi tulikuwa tukizungumzazungumza na kucheza tu." Sema: "Mlikuwa mkimfanyia mzaha Mwenyezi Mungu na Aya zake na Mtume wake?" Msitoe udhuru (wa uwongo); umekwisha kudhihiri ukafiri wenu baada ya kule kuamini kwenu (kwa uwongo). (9:64-66)


Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni hali moja; huamrisha yaliyo mabaya na huyakataza yaliyo mazuri, na kuizuilia mikono yao (hawasaidii mambo ya kheri); wamemsahau Mwenyezi Mungu (wamepuza amri Zake); na


Yeye pia amewasahau (amewapuza). Hakika wanafiki ndio wavunjao amri.Mwenyezi Mungu amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri, moto wa Jahannamu kukaa humo daima.Huo unawatosha (kuwaadhibu); na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu itakayodumu. (9:67-68)Sifa za Wanafiki zilizoainishwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo:
(i)Huepa jukumu la kupambana na maadui wa Uislamu kwa kutoa nyudhuru za uongo.
(ii)Nyoyo zao zina shaka, kwa hivyo wanasita sita kwa ajili ya shaka yao.
(iii)Huchochea fitna baina ya Waislamu.
(iv)Wanachukia mafanikio ya Waislamu.
(v)Waislamu wanapopatwa na msiba hufurahia.
(vi)Huendea swala kwa uvivu.
(vii)Wanapotakiwa watoe mali kwa ajili ya Allah (s.w), hutoa kwa kuchukia.
(viii)Huapa kwa jina la Allah kuwa wapo pamoja na Waislamu. Kihalisia hawapo pamoja na Waislamu bali wao ni maadui wa Waislamu.
(ix)Ni waoga. Wanaogopa kufa.
(x)Mgao wa zakat na sadaqat ukiangukia kwao hufurahia lakini ukienda kwa wengine wanaostahiki zaidi kuliko wao hukasirika na kunung'unika.
(xi)Wanamuudhi Mtume (viongozi) kwa kumtukana na kumkejeli.
(xii)Wanaogopa kudhihirishwa uovu wao waliouficha vifuani mwao.
(xiii)Humfanyia mzaha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. (xiv)Huamrisha mabaya na kukataza mema.
                   


           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 301


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Taathira ya Imani ya Malaika katika maisha ya kila siku
Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini. Soma Zaidi...

Kwa nini Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa
Kwa nini uislamu ndio dini pekee ya haki ambayo watu wanatakiwa waifuate. Soma Zaidi...

Shirk na aina zake
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

mitume
Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

Maisha ya Mitume
Soma Zaidi...

Kuwafanyia Wema Wazazi
Allah (s. Soma Zaidi...

Dalili (Alama) za Qiyama
Soma Zaidi...

Njia ambazo Allah hufundisha wanadamu elimu mbalimbali
Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu? Soma Zaidi...

Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

vigawanyo vya elimu
Soma Zaidi...