Posti hii inahusu magonjwa ya zinaa, ni magonjwa yanayosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana pasipo kutumia kinga au kwa lugha nyingine tunaita ngono zembe.
1. Pamoja na kuwepo kwa magonjwa haya ya zinaa Kunaa mambo yanayochangia zaidi kuwepo na kuenea kwa magonjwa haya kutoka kizazi hata kizazi na ingawa kwa kuwepo kwa dawa na elimu kuhusu ugonjwa huu lakini bado maambukizi yapo , kwa hiyo yafuatayo ni mambo yanayosababisha kuwepo kwa magonjwa haya .
2. Kujamiiana na watu mbalimbali.
Kuna watu ambao wanajaamiana na watu tofauti tofauti bila kutumia kinga hali ambayo usababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa, kwa sababu Kuna vijana ambao Wana wachumba zaidi ya mmoja na pia hawatumii kinga na wakati mwingine Kuna tabia ya kufanya ngono na wanawake wanaouza miili yao bila kutumia kinga hali ambayo usababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa.
3. Mila na desturi.
Kuna baadhi ya Mila na desturi za baadhi ya jamii usababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa, kwa mfano tabia ya kukuketa wanawake ambapo unakuta wembe mmoja unatumika kwa akina dada zaidi ya mmoja ikitokea mmoja ana ugonjwa huo usababisha wengine kupata, na pia Kuna tabia ya kurithishwa wanawake endapo mme wake amefariki hali ambayo usababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa Kama aliyefariki alikuwa na ugonjwa huo.
4. Kuwepo na vita au makazi ya wakimbizi.
Kwa wakati mwingine kuwepo kwa vita usababisha watu kuishi kama wakimbizi na wakati mwingine kuwepo kwenye kambi Moja unakuta wengine wanakuwa hawana wake zao au hawana waume zao kwa hiyo uanza kujamiiana endapo mmoja akiwa na ugonjwa huu akajamiiana na mwingine anaweza kupata magonjwa, kwa hiyo tunapaswa kutoa elimu na kuwepo kwa kinga kwenye kambi za wakimbizi.
5. Pia Kuna sababu ya umri.
Kwa wakati mwingine umri unaleta shida hasa kwa vijana ambao wameanza kubarehe kuanzia miaka kumi na mitano na kuendelea wanakuwa na wapenzi wengi hali inayosababisha kuwepo kwa ugonjwa wa zinaa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Ni ngumu kujuwa vidonda vya tumbo uhakika wake bila ya kupata vipimo. Unajuwa ni kwa nini, ni kwa sababu maumivu ya tumbo ni dalili ya shida nyingi za kiafya kama ujauzito, mimba, typhod, na shida kwenye unfumo wa chakula.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...Zijuwe dalili kuu 7 za vidonda vya tumbo, kama kiungulia, tumbo kujaa, maumivu ya umbo..
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na saratani za tishu ambazo kitaalamu hujulikana Kama Leukemia kawaida huhusisha seli nyeupe za damu. Seli zako nyeupe za damu ni wapiganaji hodari wa maambukizo - kwa kawaida hukua na kugawanyika kwa utaratibu, kadri mwi
Soma Zaidi...Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Maumivu ya mgongo yanaweza kuwa ni dalili inayoonyesha tatizo fulani la kiafya ikiwemo magonjwa au majeraha.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za kizunguzungu zinazotekea katika mwili wa binadamu
Soma Zaidi...NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO Kwa kuwa tumekwisha kuona namna ambavyo minyoo huenezwa, hivyo basi ni rahisi sasa kutaja namna ya kubambana na minyoo.
Soma Zaidi...MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGOFigo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili.
Soma Zaidi...