Njia za jumla za kujikinga na magonjwa mbalimbali
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa, kwa kawaida tunajua wazi kuwa magonjwa yapo na yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mengine hayasambai yanaweza kumpata mtu mmoja akapona au magonjwa mengine si ya kupona
Njia za kujikinga na magonjwa.
1. Njia ya kwanza ni kufanya usafi wa mazingira,kufanya usafi wa binafsi yaani kuoga, kufua nguo, kukata kucha, kusafisha meno, kunywa maji safi na salama na mambo hayo ya kuhakikisha mwili unakaa kwenye hali ya usafi kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata magonjwa,na pia kwa upande wa mazingira, kukata nyasi zilizozunguka makazi , kumchoma takataka,kutunza uchafu sehemu Moja na kutoruhusu kuishi sehemu Moja na wanyama, yaani kuwatengea wanyama sehemu yao kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata magonjwa.
2. Kupata kinga ya mwili.
Kwa upande wa kupata kinga ya mwili ni pamoja na kupata chanjo zote zinazohitajika mwilini hasa hasa kwa watoto kwa kufanya hivyo tunazuia magonjwa ambayo yanaweza kutokea hapo mbeleni,kwa mfano kupata chanjo ya kifua kikuuu, kupata chanjo ya kuzuia kupooza, kupata chanjo ya kuzuia kuharisha kupata chanjo ya pepo punda na chanjo zote za lazima kwa mtoto na kwa mabinti wanaotegemea kubeba mimba kupata chanjo zinazohitajika Ili kuepuka magonjwa mbeleni. Kwa kuweka mwili katika hali ya kinga ni vigumu kupata magonjwa.
3. Kula mlo kamili.
Kuna msemo usemao kwamba chakula Bora ni dawa, kwa sababu mlo ukiwa kamili na kutosha ni vigumu sana kupata magonjwa, kwa mfano aina zote za vyakula zikiwa sawia ni vigumu kupata magonjwa kwa mfano matumizi mazuri ya vyakula vya wanga, protein, mafuta kidogo na mboga za majani za kutosha na kunywa maji kulingana na uzito wako kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata magonjwa, lakini Kuna tabia ambayo watu wanapendelea aina Moja ya vyakula hasa vyakula vya madukani vilivyojaa kemikali na mafuta kwa wingi sukari wakitegemea kupata afya njema kwa kufanya hivyo matokeo yake ni kinenepeana na kuwa na vitambi hatimaye magonjwa ya presha na mengine mengi tu. Kwa hiyo kula mlo kamili ni kujikinga na magonjwa.
4. Kuangalia afya Yako mara kwa mara.
Kitendo cha kuangalia afya mara kwa mara nayo ni hatua Moja kubwa kwa sababu unaweza kukuta Kuna ugonjwa upo na ujautibu au kwa wakati mwingine ukikutwa na presha labda inaelekea kuwa juu unarekebisha mtindo wa maisha au ukikuta sukari ni kubwa unapunguza kiwango cha sukari kwa kufanya hivyo ni vizuri kabisa kuepuka na magonjwa au kwa vijana ni vizuri kabisa kupima maambukizi na magonjwa ya zinaa ikitokea kuna ugonjwa ni kuanza dawa mapema Ili kuweza kuepukana na matatizo mbalimbali ambayo ni pamoja na ugumba kama Kuna zinnia Kali au kuepuka kinga ya mwili kushuka kama Kuna maambukizi ya virus vya ukimwi.
5. Elimu kutolewa kila mara.
Kwa kupitia watu mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu ni jambo zuri na la busara kwa sababu pengine Kuna mlipuko Fulani wa magonjwa jamii ikijulishwa mapema na kuweza kujikinga na kufuata mashart au tiba kama ipo ni vigumu kupata magonjwa kwa hiyo viongozi wa jamii wawe tayari kutoa elimu kwa waliowazunguka Ili kuzuia kuongezeka kwa magonjwa.
6. Kutibu magonjwa kama yapo.
Njia nyingine ya kupunguza magonjwa ni pamoja na tiba kama Kuna ugonjwa Fulani kwenye jamii ni vizuri kutibu ugonjwa huo Ili kuepuka kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa sababu Kuna watu wenye kinga ya hali ya juu ana ugonjwa ila haoneshi dalili ni vizuri kutoa ushauri na kuhakikisha kuwa ugonjwa unatibika kwa watu wenye hali ya hivyo.
7. Kutumia dawa endapo Kuna maambukizi.
Ni vizuri kabisa na jambo zuri kutumia dawa ikiwa umefanya vipimo na kugundulika una maambukizi kwa mfano watu wenye maambukizi ya virus vya ukimwi ni vizuri kabisa kutumia dawa na wasione aibu kabisa kwa sababu wasipotumia dawa wanaweza kuwa na magonjwa nyemelezi yanayosababisha afya zao kuyumba.
8. Kwa hiyo kuzuia kupatwa na magonjwa ni kazi inayoweza kufanikiwa zaidi kwa kuhakikisha mazalia ya wadudu wanaosambaza magonjwa kuharibiwa kwa mfano kujaribu mazalia ya mbu, nzi na wadudu wote ambao tnajua kazi zao ni kusambaza magonjwa tunaweza kutumia njia zozote pamoja na kutumia dawa za madukani za kuua wadudu.
9. Kwa hiyo kwa kufanya hayo yaliyojadiliwa magonjwa yanaweza kupungua au yasiwepo kabisa kwa sababu magonjwa yanakuwepo kwenye jamii kwa sababu ya kutozingatia tuliyoyajadili ambayo ni kutokula mlo kamili, tabia ya kutoangalia afya zetu, kushindwa kutumia dawa baada ya vipimo,kutofanya usafi kwenye mazingira yetu,kuishi na wadudu wanaosababisha ugonjwa na mambo mengine kama hayo, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuziangatia hayo Ili tuwe mbali na magonjwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 web hosting 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
IJUE HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV) DALILI ZAKE, TIBA YAKE, CHANJO YAKE, NA MBU ANAYESAMBAZA HOMA HII
Haya ni maradhi ambayo husambazwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu kwa kupitia mbu.
Soma Zaidi...Mambo yanayochangia katika makuzi ya mtoto
Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia katika makuzi ya mtoto, mtoto katika makuzi yake anahitaji kutunzwa vizuri Ili akue kwa afya nzuri bila magonjwa
Soma Zaidi...Kiungulia na tiba zake kwa wajawazito.
Posti hii inahusu kiungulia kwa wanawake wajawazito na tiba yake, ni ugonjwa au hali inayowapata wajawazito walio wengi kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Athari za unywaji pombe na sigara wakati wa ujauzito.
Ujauzito ni kipindi muhimu ambacho afya ya mama huathiri moja kwa moja ukuaji na ustawi wa mtoto aliye tumboni. Makala hii inachunguza kwa kina madhara ya kiafya yanayotokana na matumizi ya pombe na sigara wakati wa ujauzito. Tunajadili jinsi vitu hivi vinavyovuka kizuizi cha plasenta (placenta) na kuathiri mfumo wa neva, viungo, na ukuaji wa mtoto, huku tukitoa ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuacha tabia hizi kwa ajili ya usalama wa mtoto na mama.
Soma Zaidi...Maradhi ya Ini na dalili zake, na vipi utajikinga nayo
MAGONJWA YA INI NA DALILIZAKE, NA KUKABILIANA NAYO Ini ni katika viungo vikuu katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Aina ya Magonjwa ya akili
Unyogovu (Depression ) ni mojawapo ya ugonjwa wa akili ambao unahusishwa na hisia za huzuni, kukosa matumaini, na kupoteza furaha au shauku katika shughuli za kila siku. Huu si tu hisia ya huzuni iliyokatisha tamaa, bali ni hali sugu inayoweza kuathiri mabadiliko ya mwili, mawazo, na tabia ya mtu. Unyogovu unaweza kutokea kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kemikali katika ubongo, maumbile, mazingira, na matukio mbali mbali katika maisha ambayo kupelekea mgonjwa kuwa hivyo.
Soma Zaidi...